Mchana wa leo, nilipita Mtaa wa Azikiwe Jijini Dar pale karibu kabisa na raundi abauti ya Bismini na kukutana na kibao hiki cha kinachokataza kukatiza sehemu moja ya njia kikionekana namna hii, nikapitisha lundo la Maswali kichwani kwangi, lakini sikupata jibu likilokuwa sahihi.
Nikasogea mpaka kwenye kibao hicho na kuanza kukiweka sawa kibao hicho, ambapo nilibaini kuwa skrubu moja imetoweka na ndio maana kibao hicho kimekaa namna hiyo.(sasa sijui hawakioni au ni makisudi tu)
Nikakiweka sana na kuendelea na kuendelea na mambo yangu ya kuendeleza libeneke la Mtaa kwa Mtaa.




No comments:
Post a Comment