Mtaa Kwa Mtaa Blog

amsha amsha za Kili Music Tour 2013 ndani ya Mkoa wa Kigoma

Kundi la kwanza la wasanii watakaotumbuiza katika tamasha la Kilimanjaro Music Tour 2013 limewasili mkoani Kigoma kwa ajili ya onyesho hilo. Wasanii hao 8 ni kati ya 12 watakaopanda katika jukwaa moja uwanja wa Lake Tanganyika siku ya Jumamosi.

Kundi la pili la wasanii ambao ni Profesa Jay, Diamond, Lady Jaydee na Barnaba wanatarajiwa kuwasili siku ya Jumamosi asubuhi.

Baada ya kupata mlo wa mchana ulioandaliwa na mwenyeji wao ambaye ni Doctor Gerrard Mipango wasanii hao walipata nafasi ya kutembelea makumbusho ya Doctor Livingistone yaliyoko Ujiji na kujionea historia mbalimbali ya mzungu huyo anayetambuliwa kama mvumbuzi wa Ziwa Tanganyika na pia kuona maeneo biashara ya utumwa ilipokuwa ikifanyika na kujifunza kuhusu asili ya wenyeji wa Mkoa wa Kigoma.
Wasanii wakiwa katika eneo la mbele ya makumbusho ya Doctor Livingstone.
Wakali wa muziki katika picha ya pamoja na wenyeji wao mkoani Kigoma.
Mwasiti akisoma njia zilizotumika wakati wa biashara ya utumwa.
Fid Q, Kala Jeremiah na DJ Choka eneo la abiria waliowasili uwanja wa ndege.
Fid Q kama anajaribu kuwapatanisha Dr Livingstone na mwenzake.
Wasanii wakipata mlo wa mchana nyumbani kwa Askofu Gerrard Mipango mjini Kigoma.
Baada ya kufanya ziara wasanii walipata nafasi ya kufanya manunuzi katika soko la Kigoma.
wasiti katika picha ya pamoja na mashabiki waliomuomba.
Mashabiki hawa hawakutaka kupoteza nafasi ya kuonyesha upendo kwa Fid Q.
Wasanii wakirejea kwenye basi lao ambalo lilikuwa limezongwa na mashabiki.Picha na Mdau Shaffiq.

Post a Comment

KAMERA YA MTAA KWA MTAA

[KAMERA YA MTAA KWA MTAA][carousel2]

HABARI

[HABARI][fbig1]

SHEREHE

[HARUSI][gallery1]

MKCT

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget