Waziri wa Habari. Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt Fenella Mukangara akikata utepe kuashiria Mpango wa Goal umezinduliwa rasmi.
Waziri wa Habari. Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt Fenella Mukangara kulia na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered Tanzania Bibi Liz Lloyd kulia wakifurahi baada ya kuzindua rasmi Mpango wa Goal jana jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari. Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt Fenella Mukangara akicheza mpira wakati wa hafla ya uzinduzi wa mpango wa Goal jana jijini Dar es Salaam katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Zanaki.Mpango huo umelenga kuwajengea uwezo vijana hususan wanafunzi kujitambua, kujiamini na kulinda afya zao kwa kutumia michezo.
Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari Zanaki wakifuatilia michezo mbalimbali iliyokuwa inaonyeshwa katika hafla ya uzinguzi wa Mpango wa Goal jana jijini Dar es Salaam. Mpango huo unafadhiliwa na Benki ya Starndard Chartered Tanzania.
Baadhi ya walimu wa michezo waliopatiwa mafunzo kwa ajili ya mpango huo wakifuatilia michezo mbalimbali iliyokuwa inaonyeshwa katika hafla ya uzinduzi wa Mpango wa Goal jana jijini Dar es Salaam.
Kutoka kushoto ni Waziri wa Habari. Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt Fenella Mukangara, Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered Tanzania Bibi Liz Lloyd na Mkuu wa Shule ya Sekondari Zanaki Rehema Funzo wakielekea kwenye eneo ambapo Waziri atakata utepe kuzindua rasmi Mpango wa Goal.
Waziri wa Habari. Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt Fenella Mukangara kulia na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered Tanzania Bibi Liz Lloyd wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya walimu wa michezo waliokabidhiwa vyeti baada ya kuhitimu mafunzo maalum kwa ajili ya mpango wa goal jana jijini Dar es Salaam.
Picha Zote na Frank Shija - Maelezo








No comments:
Post a Comment