HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, July 12, 2013

TPDC yapata nyongeza ya kwanza ya leseni ya utafutaji mafuta na gesi

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo akishikana mikono na Meneja wa kampuni ya AFREN kwa kanda ya Afrika Mashariki Bw.Jeremy Martin baada ya kusaini nyongeza ya kwanza ya leseni ili kuruhusu kampuni hiyo kuendelea kazi za utafutaji mafuta na gesi katika nchi kavu na kina cha bahari mashariki mwa Tanga. Kampuni ya AFREN imepata kibali cha kuendelea na shughuli za utafutaji mafuta na gesi katika eneo hilo kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC).
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akisaini nyongeza ya kwanza ya leseni ya utafutaji mafuta na gesi katika nchi kavu na kina cha bahari mashariki mwa Tanga) wanaoshuhudia ni wajumbe kutoka Bodi ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Watendaji wa TPDC, na watendaji kutoka kampuni ya AFREN.

Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) limepewa nyongeza ya kwanza ya leseni (miaka minne) itakayoliwezesha Shirika hilo kuendelea na shughuli za utafutaji mafuta na gesi katika eneo la kina cha bahari na nchi kavu Mashariki mwa Tanga baada ya leseni ya awali kuisha muda wake.

Leseni hiyo imetolewa na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo baada ya kuridhishwa na kazi za utafutaji mafuta na gesi zinazoendelea katika eneo hilo zinazofanywa na TPDC kwa kushirikiana na kampuni ya AFREN ya Uingereza.

Kutolewa kwa nyongeza ya kwanza ya leseni kutamwezesha mkandarasi kampuni ya AFREN mwenye ubia na TPDC kuendelea na shughuli za utafutaji mafuta na gesi katika eneo hilo ikiwa ni pamoja na kuchimba kisima cha utafiti katika eneo la kina cha bahari mashariki mwa Tanga ifikapo katikati ya mwaka 2014.

Kampuni ya AFREN imepewa kazi ya ukandarasi wa utafutaji mafuta na gesi katika eneo hilo kutokana na kufanya kazi nzuri ya kukusanya data za kijiolojia na kijiofizikia ambazo ziliwezesha kutambua maumbile ya kijiolojia yenye viashiria vya kuwapo mkusanyiko wa mafuta au gesi katika eneo la Tanga.

Utolewaji wa leseni hiyo ulishuhudiwa na Bodi ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), watendaji wa Wizara, watendaji wa TPDC, na watendaji wa kampuni ya AFREN.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad