HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, July 12, 2013

NENO LA LEO: UMAKINI NI MUHIMU SANA HASA KATIKA MAMBO NYETI......

Angalia kosa dogo linavyoweza kuleta madhara makubwa! Harusi ya pedeshee mmoja ilitumbukia nyongo mara baada ya uzembe na kutokuwa makini katika kutimiza majukumu kulikofanywa na mtengeneza keki maarufu sana jiji. 

Mkasa huu ulianza pale mtaalamu huyo wa kuoka keki alipoambiwa atengeneze keki nzuri sana na kisha aiandike 1 YOHANA 4:18 kwa juu!Kwa bahati mbaya, mwokaji huyo wa keki alifanya kosa la kuondoa 1 inayotangulia kabla ya neno YOHANA hivyo akaandika YOHANA 4:18.

Aidha badala ya kuandika 1 YOHANA 4:18 inayosema, “KATIKA PENDO HAMNA HOFU; LAKINI PENDO LILILO KAMILI HUITUPA NJE HOFU, KWA MAANA HOFU INA ADHABU; NA MWENYE HOFU HAKUKAMILISHWA KATIKA PENDO” jamaa akaandika YOHANA 4:18 inayosema, “KWA MAANA UMEKUWA NA WAUME WATANO, NAYE ULIYE NAYE SASA SI MUME WAKO, HAPO UMESEMA KWELI.”

Baada ya sherehe ya harusi kuisha, maharusi walielekea nyumbani na jambo la kwanza lilikuwa kusoma ule ujumbe uliokuwa umeandikwa kwenye keki yao waliyokuwa wamepewa kama zawadi. Kila mmoja wao akafungua MSAHAFU WA BIBLIA na kukutana na maneno haya, “KWA MAANA UMEKUWA NA WAUME WATANO, NAYE ULIYE NAYE SASA SI MUME WAKO, HAPO UMESEMA KWELI.” Muda uo huo mirindimo ya ngumi ikaanza kusikika na ndoa ikavunjika usiku uo huo!

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad