Kongamano la siku 3 kujadili dawa bandia limefunguliwa leo na naibu waziri wa afya, Mheshimiwa Dr. Seifu Rashid. Kongamano hili linahudhuruwa na washiriki kutoka nchi mbalimbali Africa zikiwamo Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Malawi, Botswana, South Africa, Zambia, Eritrea, Ethiopia, Madagascar, Zimbabwa, Namibia na Mozambique. Pia kuna wawakilishi toka USA na makao makuu ya shirika la afya dunia (WHO).
Wajumbe wa kongamano watapata nafasi ya kujifunza mfumo mpya wa kompyuta wa jinsi ya kutoa na kupata taarifa mbalimbali juu ya dawa bandia.
Kongamano linafanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Wakala wa Serikali wa Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (TaGLA), uliopo Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM).
Mr Hiiti B. Sillo, Mkurugenzi wa TFDA akitoa utangulizi wakati wa ufunguzi wa kongamano hilo.
Naibu waziri, Dr. Seifu Rashid akifungua rasmi kongamano hio, kulia kwake ni Michael Deats, kutoka makao makuu Shirika la Afya Duniani (WHO)
Sehemu ya washiriki wa kongamano.
Nchi za Africa zinazowakilishwa kwenye kongamano hilo.

.png)
.png)
.png)
.png)
No comments:
Post a Comment