HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, July 29, 2013

Mtuhumiwa wa wizi anusurika kufa baada ya kupokea kichapo heviii toka kwa wananchi wenye hasira kali

 Akisulubiwa kwa bakora na mmoja wa watu wenye hasira.

MTU mmoja aliyetuhumiwa kuwa ni mwizi amenusurika kufa baada ya kundi la wananchi kumpa kipigo cha maana, leo mchana katika eneo la Mbezi-Darajani, Kawe mjini Dar es Salaam. Mtu huyo ambaye jina lake halikueza kupatikana mara moja inadaiwa alikutwa akiruka geti kuingia ndani kwenye nyumba ya mkazi moja wa eneo hilo. Picha zifuatazo ni baadhi ya matukio wakati mtuhumiwa huyo alipokuwa akipata kichapo hicho.  
 Akisulubiwa kwa bakora na mmoja wa wananchi hao wenye hasira.
 Mtuhumiwa wa wizi akiomba kusamehewa wakati mtu mwenye hasira akijiandaa kumtupia tofali kichwani ambalo lilimjeruhi vibaya mtuhumiwa huyo
 Akiendelea kuslubiwa wakati wakipelekwa polisi.
 Mwenye hasira akimsulubu mtuhumiwa huyo kwa kumtandika teke.
Lakini kutokana na kipigo akaanguka hadi hatua iliyofanya watu hao wenye hasira kutawanyika eneo la tukio, wakidhani mtuhumiwa amekufa. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad