HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, July 20, 2013

Miili ya Askari Saba waliofariki huko Darfur yawasili nchini leo

Sehemu ya Masanduku yenye miili ya askari wa saba wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliofariki dunia hivi karibuni huki Darfur nchini Sudani wakati wakilinda amani,yakishushwa kwenye Ndege mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere,Jijini Dar es Salaam leo alasiri.
Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakiwa wamebeba moja ya masanduku saba yenye miili ya askari wa jeshi hilo waliofariki duni Darfur wakati wakilinda amani, baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere, Dar es Salaam leo alasiri.
Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakipakia  moja ya masanduku saba yenye miili ya askari wa jeshi hilo waliofariki dunia huko Darfur nchini Sudan wakati wakilinda amani, baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere, Dar es Salaam leo alasiri.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad