Tazama taswira za Maonyesho ya Agri-finance fair yanayoendelea hivi
sasa kwenye viwanja vya nane nane Njiro-Arusha. Maonyesho haya
yameandaliwa na TAHA USAID, SNV, TRIAS, FERT, AGRI-FOCUS, TCCIA, FARMERS
PRIDE, SMART DEVELOPMENT WORKS.
Lengo kuu la maonyesho haya ni
kuunganisha Wakulima na Taasisi za fedha ambazo zinatoa mikopo kwa
wakulima kwa ajili ya kilimo cha biashara.
Banda la Tanzania Horticultural Association TAHA
Banda la maonyesho la TRIAS
Mgeni
rasmi Bi. Chiku Issa, Mkurugenzi tawi la CRDB Arusha akipewa maelezo na
mkurugenzi wa TAHA Bi. Jacqueline Mkindi kuhusu shughuli za TAHA kwa
wakulima wa Horticuluture.
Wakulima
wakipita kwenye mabanda ili kujua huduma nzuri ya mikopo kwa wakulima
inayotolewa na taasisi za fedha zilizohudhuria kwenye maonyesho.
Wataalamu wa masuala ya mikopo kwa wakulima kutoka TRIAS wakitoa maelezo kuhusu huduma zao kwa wakulima







No comments:
Post a Comment