HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, June 2, 2013

Mwili wa Mangwea hautawasili nchini leo mpaka hapo taarifa nyingine itakapotolewa

Kamati ya msiba wa Marehemu Albert Mangweha tunaomba kutoa ya taarifa kwamba mwili wa Ndugu yetu Albert Mangwea hautoweza kufika siku ya jumapili ya tarehe 2/ 06/2013 kama ilivyo taarifa hapo awali, hii ni kutokana na sababu zilizokuwa nje ya uwezo wetu. 

 Kwa sasa tunasubiri taarifa kamili kutoka kwa wenzetu/wawakilishi wetu waliopo nchini Afrika Kusini, mara tutakapopata taarifa hizo tutawafahamisha zaidi. 

 Tunaomba radhi watanzania wote kwa usumbufu wote uliojitokeza tushirikiane na uvumilivu kwa hili. 

 Asante 

 Mwenyekiti wa Kamati 
 Kenneth Mangweha ………………………………… 
 Msemaji wa Kamati 
 Adam Juma ……………………….

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad