Akikabidhi vifaa hivyo Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe alisema, ‘‘ Bila ubishi Simba na Yanga ndio klabu kubwa za mpira Tanzania na zote zimefika katika fainali za mchuano wa Kombe la Kagame kwa mara ya 19 sasa, haya ni mafanikio makubwa kwa hizi timu, kama wadhamini wakuu wa timu hizi, Kilimanjaro Premium Lager inaziunga mkono Simba na Yanga katika harakati zao kucheza tena fainali za michuano hii ya kusisimua na ya kihistoria.
Aliongeza kuwa Kombe la Kagame ni mashindano makubwa Africa mashariki na kati, na ni jukwaa bora kwa wachezaji wetu kuonyesha vipaji vyao dhidi ya wachezaji wa viwango vya juu katika kanda hii lakini pia ni jukwaa zuri kwa wale wanaounda timu za taifa kuchagua wachezaji.
Tutaendelea kusaidia timu hizi, na kuhakikisha tunapeleka mpira wa nchi hii kwenye kilele cha mafanikio.
Meneja wa Bia ya Kilimanjaro pia aliwataka Simba na Yanga kuhakikisha wanaiwakilisha nchi yetu vizuri katika mchuano huu mkubwa wa vilabu katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati na kuwasihi kuchukua ushindi na kurudi na kombe la 12 la Kagame kwa mashabiki wanaosubiria kwa hamu.
No comments:
Post a Comment