Kwa wale wasafiri watumiao barabara ya Morogoro - Dodoma basi ni lazima watakuwa wanalifahamu vyema kabisa eneo hili la Kongwa lililopo barabarani kabisa ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa,Mkoani Dodoma.eneo hili ni maarufu sana kwa kuchoma nyama ya mbuzi na hata ya ng'ombe pia.Watu wengi hupenda kusimama katika eneo hili kwa ajili ya kupata nyama choma ambayo inachomwa kwa umaridadi mkubwa.pichani ni Nyama ikiendelea kuiva jikoni.
Wadau wakipata nyama choma katika eneo hilo.
Hapa unapata Moyo wa Mbuzi,Utumbo,maini na kadhalika.
Watu kibao wakisubiria nyama.
Mmoja wa wauzaji wa nyama hizo akifanya vitu vyake harakaharaka ili kuhakikisha wateja hawapiti mezani kwake.
Kitu kikipigwa panga.
Mjamaa akinyunyizia mambo yake kwenye nyama.








No comments:
Post a Comment