HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, June 26, 2013

akamatwa kwa sangoma kwa tuhuma za kutaka kuuwa kwa ushirikina.

 Mtuhumiwa akiwa ndani ya  chumba cha mganga na Mganga wake aitwae Yahaya tayari kwa kufanya mambo ya kishirikina.

Mama mmoja pichani juu ajulilikanae kwa jina la Magreth Simon Nkwera,  amekamatwa kwa Mganga wa kienyeji akijaribu kutekeleza jaribio la kutaka kuwauwa baadhi ya watoto wa mumewe na baadhi ya ndugu zake huko kibaha maili moja mkoani Pwani na hivi sasa yupo katika kituo cha polisi Maili moja akisubiri kupandishwa kizimbani.  
 Mtuhumiwa huyo akiwa ndani ya gari la polisi baada ya kukamatwa akiwa na huyo Mganga wa Kienyeji. 
Mtuhumiwa  ambaye ni mfanyakazi wa shirika la Nyumbu kibaha mkoani Pwani,akiwa anahojiwa na mzee wa ukoo wa Shirima,Afisa polisi jeshi daraja la Kwanza (woii mstaafu) Joseph Shirima mara baada ya kumkamata live kwa sangoma.Habari hii imetolewa na mwenyekiti wa ukoo wa shirima bwana Godilisten Hendrick Shirima.

1 comment:

  1. hakuna anayemkamata mchawi kaka yy hajihusushi na uchawi,so i just hope huyo mzee wa ukoo ni balaa na iweje hadi kamera zimfuate nyumbani kwa mganga.Kuna mashaka nahisi hao wanaomtuhumu wana bif nae la mda na pia nao wanajihusisha sana na ushirikina.Duuh sheria haina sababu ya kuingilia mambo hayo.Hizo nadhan ni bif za kiukoo na ukifuatilia sana sana utakuta kuna kitu wanagombania kama si ardhi basi mali

    ReplyDelete

Post Bottom Ad