HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, May 2, 2013

SAFARI LAGER YAKABIDHI VIFAA VYA MICHEZO KWA VYUO SHIRIKI VYA MASHINDANO YA POOL KWA VYUO VYA ELIMU YA JUU MKOANI IRINGA

Meneja wa Kampuni ya Bia Tanzania(TBL) Mkoa wa Iringa, Josephat Changwe (kushoto) akimkabidhi tisheti Diwani wa Kata ya Kitanzini Manispaa ya Iringa Mjini, Jesca Msambatavangu ili awakabidhi vyuo shirika vya elimu ya juu kwenye mashindano ya Pool kwa vyuo hivyo Iringa jana.Kulia ni Mwenyekiti wa chama cha Pool Mkoa wa Iringa Salum Kisaku.
Diwani wa Kata ya Kitanzini Manispaa ya Iringa Mjini, Jesca Msambatavangu (kushoto) akimkabidhi tisheti nahodha wa timu ya chuo Kikuu cha Ruaha, Said Mohamed wakati wa hafla fupi ya kukabidhi vifaa vya michezo kwa vyuo shiriki vya mashindano ya Pool kwa Vyuo vya Elimu ya Juu Mkoa wa Iringa.Katikati Kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Pool Mkoa wa Iringa,Salumu Kisaku na Katibu wa chama hicho,Haji Kiyeyeu.
Diwani wa Kata ya Kitanzini Manispaa ya Iringa Mjini, Jesca Msambatavangu(wa pili kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa hafla fupi ya kukabidhi vifaa vya michezo kwa vyo shiriki vya mashindano ya Pool yanayotarajiwa kuanza kesho Mkoa wa Iringa.Kushoto ni Meneja wa Kampuni ya Bia Tanzania(TBL) Mkoa wa Iringa, Josephat Changwe.Kutoka kulia ni Katibu wa chama cha pool Mkoa wa Iringa,Haji Kiyeyeu na Mwenyekiti wa chama hicho,Salum Kisaku.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad