Afisa wa Mfuko wa Pspf Mkoa wa Lindi Bw Delphil Richard Akibainisha mafao yanayotolewa na PSPF.
Walimu Tarajari Chuo cha Ualimu Nachingwea wakipata somo kuhusiana na Mfuko wa PSPF unavyohudumia wanachama wake.
Na Abdulaziz Video
Walimu tarajiwa katika chuo cha Ualimu Nachingwea mkoani Lindi wameshauriwa kujiunga na mfuko wa penseni kwa watumishi wa umma Pindi wamalizapo mafunzo yao na kupata ajira.
Wito huo umetolewa na Afisa wa Mfuko wa Pspf Mkoa wa Lindi Bw Delphil Richard alipokuwa anazungumza na wanachuo hao kwenye semina yakutoa elimu kuhusu mfuko huo kwa wananachama wake na walimu tarajari katika chuo hicho.
Richard alisema kuwa lengo la kukutana na walimu hao watarajiwa ni kuwahamasisha kujiunga na mfuko wa PSPF na kutoa taarifa mbalimbali ikiwemo michango na usajili wa uanachama na kubainisha kuwa mfuko unatoa mafao mbalimbali kwa wanachama wake yakiwemo ya uzeeni, ulemavu, mirathi, rambirambi za mazishi, wategemezi, na malipo ya pensheni ya kila mwezi.
Richard aliongeza kuwa pamoja na huduma hizo pia mfuko umeanzisha mpango wa uchangiaji wa hiari kwa ajili ya kupanua wigo wa uanachama kwa kuandikisha wananchi walioajiriwa au kujiajiri katika sekta rasmi na isiyo rasmi.
Kupitia mpango huo utawezesha wale wote ambao hapo awali hawakuweza kupata huduma ya hifadhi ya jamii kutokana na kutokuwa katika ajira rasmi ambapo sasa kupitia mapato yake anao uwezo wa kujiunga na PSPF
No comments:
Post a Comment