WANAFUNZI
zaidi ya 20 wa shule ya kimataifa ya St Charles iliyopo Don Bosco
katika Manispaa ya Iringa wamenusurika kifo baada ya gari
waliyokuwa wamepanda aina ya Hiace lenye namba T415 AEG kushindwa
kupanda mlima na kupinduka.
Huku
mbinu za wezi wa watoto zikionyesha kugonga mwamba baada ya
mwanamke mmoja kushtukiwa akitaka kukimbia na mtoto asiye wake kwa
madai anamkimbiza Hospitali.
Ajali
hiyo imetokea majira ya saa nane mchana wa leo katika eneo la
Msikiti wa Hidaya katika kata ya Mivinjeni katikati ya mji wa Iringa.
Wakizungumza
na mwandishi wa habari hizi eneo la tukio baadhi ya mashuhuda
walisema kuwa daladala hilo ambalo lilikuwa likitokea eneo la
Frelimo katika Manispaa ya Iringa kuelekea mjini Iringa mara baada ya
kufika eneo hilo lilishindwa kupanda mlima na kuanza kurudi nyuma
kwa kasi kabla ya kupinduka.
Alisema
shuhuda huyo Juma Omari kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi
,ubovu wa gari hilo pamoja na uzembe wa dereva ambaye alionekana
kuendesha gari hilo kwa bila kuchukua tahadhari na pamoja na kutambua
mbele kuna kona na mlima ila hakuweza kuzingatia hilo.
Hata
hivyo alisema kutokana na ajali hiyo dereva na konda wake
waliwatelekeza watoto hao ambao wanakadiliwa kuwa na umri wa miaka 7
na 9 na wao kutoweka kusikojulikana na kuwaacha watoto hao bila
kuwapa msaada wowote hadi wananchi walipofika kutoa msaada wa
kuwatoa katika daladala hilo na kuwakimbiza katika Hospitali ya
Rufaa ya mkoa wa Iringa kwa matibabu zaidi .
Alisema
katika ajali hiyo hakuna aliyepoteza maisha zaidi ya mwanamke mmoja
ambae jina lake bado kufahamika aliyejeruhiwa vibaya mikono yake.
Hata
hivyo mmoja kati ya wauguzi wa Hospitali ya mkoa wa Iringa ambae
hakutaka kutaja jina lake kwa kuwa si msemaji wa Hospitali hiyo
alisema kuwa hali za watoto hao si mbaya sana zaidi ya kupata
michubuko midogo midogo .
Diwani
wa kata ya Mvinjeni Frank Nyalusi amethibitisha kutokea kwa ajali
hiyo na kuwapongeza wananchi wa kata hiyo ambao walifika kutoa
msaada kwa watoto hao kwa kuwakimbiza Hospitali.
wakati
huo huo mwanamke mmoja ambae jina halikuweza kupatikana mara moja
amedaiwa kutka kuiba mmoja kati ya watoto waliojeruhiwa kwa madai
kuwa ni mtoto wake na alikuwa akitaka kumkimbiza Hospitali ya wilaya
ya Iringa Frelimo badala ya Hospitali ya Rufaa ya mkoa ambako majeruhi
wengine walikimbizwa .
Mwanamke
huyo alishtukiwa baada ya kukutwa akitimua mbio uchochoroni huku akiwa
na mtoto huyo na baada ya kubanwa aliamua kumtelekeza mtoto huyo na
kukimbia hali iliyopelekea uongozi wa mtaa kuomba watoto wote wale
waliojeruhiwa na wazima kukimbizwa Hospitali ya mkoa .
Wasamaria wema wakitoa msaada kwa wanafunzi wa shule ya St Chalresy Iringa waliojeruhiwa katika ajali leo .
Wanafunzi waliojeruhiwa katika ajali wakilia kwa uchungu kabla ya kukimbizwa Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Iringa
Askari wa usalama barabara wakifika eneo la tukio kutoa msaada
Wanafunzi hao majeruhi wakiwa Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Iringa
Askari wa usalama barabarani akitoa msaada kwa majeruhi wanafunzi wa St. Chalresy leo katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Iringa.
No comments:
Post a Comment