Afisa Mkuu wa Mauzo na Masoko wa TTCL Bw. Peter Ngota akionyesha
simu mpya na ya kisasa (smart phone) zinazopatikana katika vituo vyote vya huduma kwa wateje
nchini kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya BANDO NA TTCL
pamoja kampeni ya BASTI iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.kulia ni mkuu wa Mauzo Bw. Kisamba Tambwe.
Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa maendeleo ya bidhaa wa TTCL
Ernest Isaya, afisa mkuu wa mauzo na masoko Peter Ngota na Mkurugenzi wa
Mauzo Bw. Kisamba Tambwe.
Afisa mkuu wa mauzo na masoko wa TTCL Bw. Peter Ngota akionesha
bango lenye punguzo kubwa la bei ya Intanet wakati wa uzinduzi wa
kampeni ya BASTI uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.anayeshuhudia ni Mkurugenzi wa Mauzo wa TTCL, Kisamba
Tambwe.
baadhi ya Wafanyakazi wa TTCL na waandishi wa habari waliohudhulia uzinduzi.
Kampuni ya simu Tanzania (TTCL) imezindua huduma ya BANDO NA TTCL” na kampeni ya punguzo kubwa la bei ya Intanet ijulikanayo kama BASTI.
Akiongea wakati wa uzinduzi huo, Afisa mkuu wa mauzo na Masoko wa TTCL Bw. Peter Ngota amesema, baada ya kujitambulisha sokoni kwa Intanet isiyo na kikomo ya BANJUKA leo tunazonfua huduma mpya ujulikanayo kama BANDO NA TTCL. Huduma hii itamuwezesha mteja kufaidika na meseji za bila kikomo, kuperuzi intanet na muda wa maongezi kwenda mitandao yote kwa wakati mmoja kwa bei hadi ya shilingi 500.
Amesema BANDO NA TTCL inawalenga zaidi watumiaji wa simu za kisasa za smart phone za TTCL zinazopatikana katika vituo vyetu vya huduma kwa wateja nchini.
Bw. Ngota amesema TTCL pia imeshusha kwa kiwango kikubwa bei ya vifurushi vyake vya mobile intanet kwa kampeni ya BASTI ikimaanisha peruzi intanet zaidi kwa gharama nafuu. Ametolea mfano kifurushi cha mwezi cha 4GB kilichokuwa kinauzwa shilingi 90,000/= sasa kinauzwa kwa shilingi 25,000/= tu. Hii ni nafasi si tu kwa wateja waliopo wa TTCL kuongeza matumizi kwa gharama nafuu, bali hata wateja wapya ikiwamo watumiaji wadogo kujiunga na mtandao wa TTCL. (haki ya mawasiliano kwa wote).
Amesisitiza kuwa , BANDO NA TTCL na kampeni ya BASTI zina manufaa mengi ikiwa ni pamoja na huduma ya mobile intanet kwa gharama nafuu, vifurushi vya siku, wiki na mwezi kulingana na mahitaji yako, mobile intanet yenye ubora na kasi ya juu zaidi.
Amesema kwa kununua modem ya TTCL kwa sh 29,000/= utapata 2GB bure kuperuzi intanet na kukupa thamani bora kwa pesa yako.
‘Leo hii wateja wengi zaidi na hasa wanafunzi na wajasiriamali wanatumia simu za kisasa (smart phones, tablet PC’s kama iPad, Samsung Galaxy nk) na kompyuta ili kupata huduma za intaneti na mitandao ya kijamii kwa shughuli zao za kila siku.’
Aidha, kuwepo kwa mitandao ya mawasiliano ya baharini ya EASSy na SEACOM katika Pwani ya Tanzania, mkongo wa Taifa wa mawasiliano na mtandao wake ulionenea nchi nzima umeiwezesha TTCL kuwa mstari wa mbele kutoa huduma za mawasiliano ikiwamo intaneti kwa ofisi za serikali na benki mbalimbali hapa nchini.
Mkongo wa Taifa umesaidia kuwa na huduma bora zaidi ambapo kwa sasa wananchi wanaweza kupata huduma nyingi zikiwemo matibabu mtandao, elimu mtandao, biashara mtandao na Serikali mtandao, Benki – Mtandao, Pesa – mtandao na pia kufanikiwa kuifikisha Tanzania katika nchi za Zambia, Burundi, Rwanda na Malawi kwa huduma za mawasiliano.
Kama kuna shirka ninaloweza kusema hata leo life ni TTCL na hasa upande wa marketing na huduma kwa wateja.Idara inayofanya vizuri ni mafundi an wenyewe wa idara zingine.
ReplyDeleteMimi nilikuwa na TTCL ya wireless,iliharibika nikairudisha imechukua mwaka na kila nilipokuwa nikifuatilia wanasema imepelekwa idara ya ufundi Dar-es-salaam,hadi nilipotishia kupewa simu yangu ili niiharibu kwani nilishaanza kuhisi imeuzwa.Cha kushangaza iliporudi nilikuta ina password na pia ilikuwa na namba za watu ambao siwaju--kuashiria ilikuwa inatumiwa na mtu nisiyemjua.Niliporudisha wakasema inabidi tena niiacha ili wakaondoe password--ilichukua miezi mitatu--siku nafuatilia dada mmoja ananiambia aliyeipokea yuko likizo hadi arudi--sikumuelewa nikaomba kuonana na Manager--Manager akaamuru itafutwa na nipewe majibu ya maana.Walipoitafuta wakaipata--ikawa bado ina password.
Kusema kweli they dond bother to loose a customer.Ni kwa sababu wanalipwa mishahara toka serikalini na wala hawajali kwani they loose nothing.
Kuna mengi sana ya kusema ila kwa leo niishie hapo.
Patrick
Morogoro mjini
Zantel ana kifurushi cha 5GB anatoza Shs 20,000 kwa mwezi, sasa nyie TTCL na kitu gani kipya??????
ReplyDelete4GB mnataka kutoza Shs 25,000 kwa mwezi, unahitaji moyo wa mwendawazimu kuchagua huduma yenu. Mnasumbuliwa na nini???
Hivi mnaishi wapi???? Hamjiulizi mshindani wako yuko vipi sokoni kabla nawe hujaingia????
Hili shirika linatakiwa lifumuliwe na waziri husika kama wafanyavyo wengine bila kujali kitakachotokea kwani liko nyuma ya mabadiliko ya Dunia, wako mijini tu na hawaangalii kuboresha miundo mbinu vijijini!!!!!!!! wafanyakazi wengi wao ni wale wa enzi ya Baba wa taifa!!!! kulindana tu!!!!
ReplyDeletekuhusu Zantel kutoa 5GB kwa sh 20,000 na TTCL kutoa 4GB kwa 25,000 tofauti yake ni kuwa, kwa ttcl utapata speed ya kutosha ukiringanisha na Zantel pamoja na kampuni zengine za simu, kwa TTCL speed yao ya internet haina mpinzani kwa sasa, wanachomiss TTCL ni utangazaji na kuweza kujieleza kwa wateja wao.
ReplyDeleteKama wanashindwa kuangalia competitor ametoa kitu gani na mimi nitoe kitu ambacho kina bei kubwa lakini nikielezee kiasi kwamba mteja asiangalie bei bali kitu gani atapata toka kwenye hiyo pesa aliyotoa.Hawajamaa wameambukizwa usingizi wa pono na wazee waliokuwa hapo TTCL mpk wao hawajitambui kabisa.Hawajui kufanya marketing.Huyo Afisa masoko anaonekana umri wake hauendani na soko la kampuni za simu upande wa marketing lilivyo.Inabidi wafumue idara walete vijana creative ikiwezekana waibe toka kampuni zingine za mawasiliano tutawalipa sisi mishahara mizuri kwa kodi zetu.
ReplyDeleteHili shirika linahitaji mabadiliko makubwa sana hasa kwenye jinsi wanavyowafikia na kuhudumia wateja.Mimi ni mmoja wa wateja wa shirika hili nina simu kama hizo zilizo mbele za hao mabwana hapo pichani. Kuna wakati nikawa sipati connection,nikaenda ofisi yao kule posta dsm.Nikakutana na dada mmoja mfanyakazi wa hapo,nikaanza kumwelezea nina tatizo kwenye simu yangu ya mezani.Yeye pasipo hata kunisikiliza sawasawa nimwelezee nature ya tatizo,ananiambia njoo na hiyo simu kwanza ndo tutakusikiliza. Tena anajibu akiwa busy na shughuli zake zingine utafikili nimekuja hapo kumwomba msaada!
ReplyDeleteKwa kweli niliumia sana hasa ukizingatia nilikuwa na shida ya mawasiliano wakati huo.Nashukuru mashirika ya simu yapo mengi,lakini vinginevyo kama ingekuwa ni kuwategemea hawa jamaa tu,tungeumia sana.
Badilikeni TTCL.
Halafu kumbe wanatumia CDMA pekee. Nimeenda customer service office nampa huyo officer specifications za simu atambaue kama zinaendana, alichonijibu hakikunisaidia kwa kifupi kabisa. Ila kwa style hiyo hawatumuuzia mtu
ReplyDeleteje hawa jamaa wanatumia line za kawaida au????
ReplyDelete