Ile mvua iliyonyesha leo jijini Dar yenye ujazo wa kama vigudulia viwili au vitatu hivi kama sikosei,imepelekea mtaa huu uliopo maeneo ya Mikocheni "A" kujaa maji kiasi kwamba hakuna kwa kupita wala kwa kukanyaga,hali inayoleta kero kwa wakazi wa eneo hilo.pia imekuwa ikiwapa shida watumiaji wa magari ambao wengi wao hukilazimika kupita kwa shida sana kwa kuwa hakuna namna nyingine ya kufia au kutoka nyumbani..
Huyu ni mmoja wa walioipata hadha hiyo siku ya leo,na hapo ukipoteza step tu.ujue umeingia mtaroni.
Msamalia akitoa msaada tutani baada ya kuona jamaa wa gari akihaha kutafuta njia ya kupita.
No comments:
Post a Comment