Mkurugenzi mkuu wa Nhif akitoa taarifa fupi ya mfuko wa Bima ya Afya kwa Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Lindi kuhusiana na mpango endelevu wa kuleta madaktari Bingwa Mikoani
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Lindi Abdallah Ulega akikabidhi msaada uliotolewa na NHIF kwa hospital ya Sokoine.
Baadhi ya madaktari Bingwa wanaotoa tiba katika Hospital ya Mkoa wa Lindi kwa Ufadhili wa NHIF.
Kaimu mkuu wa mkoa wa Lindi,Abdallah Ulega akizungumza wakati wa kuzindua tiba ya Madaktari Bingwa toka Muhimbili watakaotoa tiba kwa wateja wa Nhif na wasio wateja hadi tarehe 13 April
Baadhi ya wadau waliohudhuria uzinduzi huo
Baadhi ya viongozi wakiwasili sokoine hospital kwa ajili ya uzinduzi wa Tiba kwa madaktari Bingwa
Na Abdulaziz Video,Lindi
Wananchi mbalimbali wa Wilaya zote Za Mkoa wa Lindi leo wameanza kupata tiba na Uchunguzi toka kwa Madaktari Bingwa wa Kizalendo toka hospital ya Taifa ya Muhimbili kufuatia ufadhili uliotolewa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ili kurahisha Huduma ya Matibabu kwa Jamii.
Huduma hizo zimeanza kutolewa leo hadi tarehe 13 mwezi huu baada ya Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Lindi,Ambae pia ni Mkuu wa wilaya ya Kilwa,Abdallah Ulega kuzindua mpango huo unaotolewa na mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kwa kuanzia Mikoa yenye Upungufu wa Madaktari Bingwa kwa kuanzia na Mkoa wa Lindi.
Akizindua mpango huo ni ambao utasaidia kuwapunguzia mzigo Wagojwa kufuata huduma Kwa madaktari Bingwa na kuchukua muda mrefu na mafanikio ya kuonana na kupata huduma stahiki.
Aidha katika Hafla hiyo,Ulega alitoa wito kwa jamii kuunga mkono jitihada hizo kwa kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii(CHF) Huku akisisita kuwa serikali itaendelea kuchangia asilimia mia kwa Michango ya Chf itakayochangwa.
‘Ndg zangu wa Lindi huu mfuko ni kwa ajili yenu ili kuwapunguzia gharama za matibabu kwa Kaya,,,Ukichangia elfu 10 na serikali inachangia elfu 10 na tumejipanga kuhakikisha huduma zinaboreka na dawa zinapatika Nawaomba Mchangamkie kuliko malipo ya papo kwa hapo kila ukiumwa lakini CHF ni mwaka mzima wewe na familia’Alifafanua Ulega.
Kwa Upande wake,Mkurugenzi mkuu wa Mfuko,Emmauel Humba Akizungumzia ujio wa madaktarihao alisema utaratibu huu unaofanywa na madaktari hao kupitia Wizara ya Afya,Sokoine Hospital na Ofisi yake unawapa fursa wananchi wa vijijini na Mjini ili kupata utaalamu wa kupimwa kuwaondoshea usumbufu wa maradhi yaliyoficha na hatimaye kupatiwa tiba.
Alitoa wito kwa wananchi wanapopata taarifa za kufikiwa na madaktari bingwa wa maradhi mbalimbali, wasipuuze kwenda kufanyiwa uchunguzi, kwani huenda wakawa wanaishi na maradhi ambayo hayajajitokeza.
Nhif imeanza huu utaratibu hasa kwa mikoa ambayo ina upungufu wa madaktari Bingwa na Tumeanzia Lindi na katika kuunga Jitihada za Mama Kikwete kuleta vifaa hii imetufurahisha sana kwa kuwa Wateja wa Mfuko wetu sasa watapata huduma bora na Vipimo,,,Naomba wateja wa Bima na wasio wateja watumie fursa ya kuonana na Madaktari hawa na wale wale wa mkoani wafike mawilayani na itakuwa zoezi Endelevu..Alimalizia Emmanuel Humba,Mkurugenzi mkuu NHIF.
Sambamba na kuishukuru Serikali kupitia NHIF,Bi Amina Machenza na Sheikh Mkuu waMkoa wa Lindi,Sheikh Mohamed Mushangani licha ya kutambua uwepo wa uhaba wa madaktari unaozikabili hospitali na vituo vya afya vilivyoko vijijini, Wameomba huduma za kuletwa kwa Madaktari Bingwa Ziwe Endelevu kwa jamii nyingi ni za kipato cha chini.
Sambamba na Madaktari hao Mfuko huo umekabidhi vifaa mbalimbali kwa hospital hiyo vyenye thamani ya Tshs Milion 20 huku Wagonjwa mbalimbali watakaojitokeza watapatiwa huduma hizo kwa kupimwa na kutibiwa maradhi ya macho, pua, kifua, masikio magonjwa ya akinamama na Watoto ikiwemo Upasuaji.
No comments:
Post a Comment