Meneja wa Ofisi ya Mfuko wa Taifa ya Bima ya Afya-Lindi,Bi Fortunata Kullaya akitoa taarifa ya ujio wa Madaktari Bingwa wanaoletwa na Mfuko huo na kuhudhuriwa na Mkurugenzi Mkuu wa NHIF kesho katika hospital ya Sokoine Lindi
Viongozi wa mfuko wa NHIF pamoja na WAMA wakiwa wameketi pamoja chini na waliohudhuria katika Elimu elekezi kwa vikundi vya wajasiriamali kujiunga na CHF Iliyofanyika katika kijiji cha Namangale-Lindi Vijijini.
Picha na Habari-Mdau Abdulaziz Video,Lindi
Mfuko
wa Taifa wa Bima ya Afya umeandaa huduma za madaktari bingwa kutoka
hospitali ya Rufaa MUHIMBILI watakaotoa huduma katika hospitali ya Rufaa
ya Mkoa wa Lindi (SOKOINE) kuanzia tarehe 8.4.2013 hadi tarehe
13.4.2013.
Uzinduzi
wa huduma hiZi utafanywa rasmi siku ya jumatatu(KESHO) tarehe
8.4.2013,Mgeni rasmi ni mkuu wa mkoa wa Lindi pia uzinduzi huo
utahudhuriwa na Mkurugenzi mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya,Ndg
Emmanuel Humba.
Akitoa
taarifa hiyo kwa Waandishi wa Habari,Meneja wa ofisi ya Mfuko wa Taifa
wa Bima ya Afya Lindi,Bi Fortunata Kullaya alieleza kuwa hatua hiyo
imekuja ili kusaidia huduma kwa wateja wa Mfuko huo na wagonjwa wengine
ambapo wagonjwa wasio wateja wa Mfuko watatumia taratibu za kawaida
zilizopo katika kupata matibabu.
Hivi
karibuni Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Kwa kushirikia na Taasisi ya
Wanawake na Maendeleo(WAMA)imetoa mafunzo kwa vikundi mbalimbali vya
wajasiliamali katika wilaya za Lindi na Kilwa ili wajiunge na mfuko wa
Afya ya Jamii(CHF) NA Kutoa msaada wa Mashuka kwa Hospital za Wilaya ya
Ruangwa na Kilwa.
No comments:
Post a Comment