Bendi ya maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya "Ngoma Africa Band" imepokea kwa udhuni na majonzi makubwa taarifa ya kifo cha mwanamuziki mkongwe barani afrika hayati Bibi.Fatuma binti Baraka (Bi.KIDUDE) mwenyezi amrehemu.
Ngoma Africa band inatoa mkono wa pole na rambi rambi kwa familia ya marehemu
Bi.Kidude,pia kwa sisi sote wanamuziki na wasanii pamoja na watanzania wote kuondokewa na Mkongwe wetu Bi.Fatuma Binti Baraka (Bi.Kidude),ambaye alikuwa
ni balozi na hadhina ya utamaduni wa mwambao na waswahili, kitaifa na kimataifa.
Marehem Bi.Kidude hakuwa msanii au mwanamuziki tu bali alikuwa mpiganaji jemedari aliyeupigania na kuulinda utamaduni wa jadi ya kiswahili na mwambao.

Ngoma Africa band itasimamisha shuguli za kutumbuiza kwa mda wa siku 10
kwa ajili ya maombolezo ya msiba wa marehemu Bi.Kidude.
Mwenyezi mungu amlaze mahala pema peponi Bibi.Fatima binti Baraka (Bi.Kidude)
Amin.
No comments:
Post a Comment