Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana jijini Mwanza,Mh. Baraka Konisaga (kushoto) akisalimiana na Meneja Mauzo na Usambazaji wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) jijini Mwanza,Andrew Mbwambo wakati alipowasili kwenye Viwanja vya Furahisha tayari kwa Hafla ya kutoa Baraka zake wa Bia ya Safari Lager iliyoshinda Tuzo ya Bia Bora Barani Afrika.Kulia ni Meneja Matukio wa TBL kanda ya Ziwa,Erick Mwayela na wa Pili kushoto ni Mdau Deodatus Katambi.
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana jijini Mwanza,Mh. Baraka Konisaga akipokea Kombe la Ushindi wa Bia Bora Barani Afrika ulioupata Bia ya Safari Lager kutoka kwa Meneja wa Bia ya Safari Lager,Oscar Shelukindo ikiwa ni kutoa Baraka zake kwa Kombe hilo kuwepo jijini Mwanza,katika hafla fupi iliyofanyika kwenye viwanja vya Furahisha jijini Mwanza leo.
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana jijini Mwanza,Mh. Baraka Konisaga akinyanyua Juu Kombe la Bia Bora Barani Afrika ulioupata Bia ya Safari Lager wakati wa kutoa baraka zake kwa ziara ya Kombe hilo jijini Mwanza.
Meneja wa Bia ya Safari Lager,Oscar Shelukindo akizungumza na wakazi wa jiji la Mwanza waliofika kwenye viwanja vya Furahisha jijini hapa kufurahia ushindi wa Bia Bora Barani Afrika ulioupata Bia ya Safari Lager hivi karibuni huko nchini Ghana.Safari Lager ipo kwenye ziara ya kutembelea Mikoa mbali mbali hapa nchini ili kufurahia ushindi huo na wanywaji wa bia hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana jijini Mwanza,Mh. Baraka Konisaga akisisitiza jambo kwa wakazi wa jiji la Mwanza waliofika kwenye viwanja vya Furahisha kusherehekea ushindi wa Bia ya Safari Lager.
Burudani ikitolewa.
Picha ya pamoha.
No comments:
Post a Comment