Wananchi wa Mtaa wa Buza Kata ya Buza Wilaya ya Temeke Mkoani Dar es Salaam wakipiga kura za kuwachagua wananchi watakaopendekezwa kuwa Wajumbe wa Mabaraza ya Katiba ya Wilaya wakati wa Mkutano Mkuu Maalum wa Mtaa huo uliofanyika katika Shule ya Msingi Buza leo.
Wagombea
wa nafasi za uwakilishi wa wanawake katika kikao cha Mkutano Mkuu
Maalum wa Mtaa Mtaa wa Buza Kata ya Buza Wilayani Temeke Mkoani Dar e
Salaam wakionyesha nambari zilizotumika kuwachagua wananchi
waliopendekezwa kuwa Wajumbe wa Mabaraza ya Katiba ya Wilaya. Kikao
hicjo kilifanyika katika shule ya Msingi Buza leo.
Mwenyekiti
wa Serikali ya Mtaa wa Shimo la Udongo Kata ya Kurasini Wilaya ya
Temeke mkoani Dar es Salaam, Issa Chigona akizungumza na wananchi wa
Mtaa huo kabla ya kufanyika kwa mkutano Mkuu Maalum wa Mtaa ili
kuwachagua wananchi watakaopendezwa kuwa wajumbe wa Mabaraza ya Katiba
ya Wilaya leo.
Wakazi
wa Mtaa wa Buza, Kata ya Buza Wilayani Temeke Mkoani Dar Es Salaam
wakifuatilia kwa makini kikao cha mkutano mkuu maalum wa Mtaa kwa ajili
ya kuchagua wananchi watakaopendekezwa kuwa wajumbe wa Mabaraza ya
Katiba ya Wilaya katika Mtaa huo leo.
Mkazi
wa Mtaa wa Mivinjeni Kata ya Kurasini Wilayani Temeke mkoani Dar es
Salaam, aliyewania nafasi ya uwakilishi wa Vijana katika Mikutano wa
Mabaraza ya Katiba ya Wilaya, Sophia Stephen akijinadi mbele ya wananchi
wa mtaa huo kabla ya kufanyika kwa kwa Mkutano Mkuu Maalum wa Mtaa ili
kuwachagua wananchi watakaopendezwa kuwa Wajumbe wa Mabaraza ya Katiba
ya Wilaya katika Mtaa huo leo
No comments:
Post a Comment