Prof. Gaspar Munishi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Idara ya Sayansi ya Siasa na Utawala akielezea kuhusu umuhimu wa kuboresha rasimu ya Sera ya manunuzi wakati wa kongamano la kujadili rasimu hiyo lililofanyika hivi karibuni katika ukumbi wa Kimataifa wa mikutano wa JB jijini Dar es Salaam. Kongamano hilo la siku moja liliandaliwa na Idara ya Sera ya manunuzi ya umma. Kulia ni Dk. Godfrey Sansa kutoka Chuo hicho.
Khamisi Tikka kutoka Mamlaka ya Rufaa za zabuni akichangia mada wakati wa kongamano la kujadili rasimu ya Sera ya manunuzi ya Umma lililofanyika hivi karibuni katika ukumbi wa Kimataifa wa mikutano wa JB jijini Dar es Salaam. Kongamano hilo la siku moja liliandaliwa na Idara ya Sera ya manunuzi ya umma na kuhudhuliwa na wajumbe mbalimbali kutoka ofisi za Serikali na Taasisi binafsi.
Emmanuel
Maliganya ambaye ni Afisa Ugavi kutoka Benki Kuu ya Tanzania akichangia
mada kuhusu utendaji kazi wa maafisa ugavi wakati wa kongamano la
kujadili rasimu ya sera ya manunuzi ya umma lililofanyoka hivi karibuni
jijini Dar es Salaam. Kongamano hilo la siku moja liliandaliwa na Idara
ya Sera ya manunuzi ya umma kuhudhuliwa na wajumbe mbalimbali kutoka
ofisi za Serikali na Taasisi binafsi.
Juma
Fimbo kutoka Umoja wa wataalamu wa Manunuzi na Ugavi Tanzania akielezea
jinsi maafisa ugavi wanavyotakiwa kufanya kazi zao kwa kutumia taaluma
ya uchumi wakati wa kongamano la kujadili rasimu ya sera ya manunuzi ya
umma lililofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam. Kongamano hilo la
siku moja liliandaliwa na Idara ya Sera ya manunuzi ya umma na
kuhudhuliwa na wajumbe mbalimbali kutoka ofisi za Serikali na Taasisi
binafsi.
Mkurugenzi
wa Ugavi kutoka Akaunti ya Changamoto za Milinia (Millenium Challange
Account) Marieth Ngaida akichangia mada wakati wa kongamano la kujadili
rasimu ya sera ya manunuzi ya umma lililofanyika hivi karibuni jijini
Dar es Salaam. Kongamano hilo la siku moja liliandaliwa na Idara ya Sera
ya manunuzi ya umma.
Kamishna
wa Idara ya Sera ya manunuzi ya umma kutoka wizara ya Fedha Dk.
Frederick Mwakibinga (kulia) akiongea jambo na Clemence Tesha ambaye ni
mjumbe wa kamati ya sera ya manunuzi wakati wa kongamano la kujadili
rasimu ya sera ya manunuzi ya umma lililofanyika hivi karibuni jijini
Dar es Salaam. Kongamano hilo la siku moja lilihudhuliwa na wajumbe
mbalimbali kutoka ofisi za Serikali na Taasisi binafsi.
Baadhi ya wajumbe kutoka ofisi za Serikali na Taasisi binafsi wakimsikiliza Prof. Gaspar Munishi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Idara ya Sayansi ya Siasa na Utawala (hayupo pichani) wakati wa kongamano la kujadili rasimu ya Sera ya manunuzi ya Umma lililofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam. Kongamano hilo la siku moja liliandaliwa na Idara ya Sera ya manunuzi ya umma.Picha na Anna Nkinda – Maelezo
No comments:
Post a Comment