HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, April 29, 2013

CRDB YAKABIDHI JENGO LA WODI YA WATOTO HOSPITALI YA MKOA WA MOROGORO

 Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid  akizindua wodi ya watoto katika hospitali ya Mkoa wa Morogoro.
 Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid (katikati) akipokea mfano wa ufunguo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya CRDB Dk. Charles Kimei wakati wa kukabidhi jengo la wodi ya watoto ya Hospitali ya Mkoa wa  Morogoro,  ambayo imefanyiwa ukarabati mkubwa na benki hiyo. Hafla hiyo imefanyika mjini Morogoro juzi. Kushoto ni Mkurugenzi wa benki ya CRDB tawi la Morogoro, Pendo Assey.
 Jengo la Wodi ya Watoto katika Hospitali ya Mkoa wa Morogoro ikionekana ikiwa katika hali nzuri baada ya kufanyiwa ukarabati na Benki ya CRDB na kugharimu kiasi cha sh. milioni 50.
 Meya wa Manispaa ya Morogoro Amir Nondo (kushoto) akifurahjia jambo na Mkurugenzi wa Masoko Utafiti na Huduma kwa Wateja, Tully Mwambapa (kati) na Mkurugenzi wa benki ya CRDB tawi la Morogoro, Pendo Assey. 
Wafanyakazi wa benki ya CRDB wakiwa wameshika miche ya miti tayari kwa kuanza zoezi la upandaji miti kuzunguka katika maeneo ya hospitali ya Mkoa wa Morogoro. 
Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid akipanda mti wa kumbukumbu baada ya uongozi wa benki ya CRDB kukabidhi jengo la wodi ya watoto katika hospitali ya Mkoa wa Morogoro lililofanyiwa ukarabati pamoja na kuwekewa vifaa muhimu katika wodi hiyo. Jumla ya Sh. Milioni 50 zimetumika katika ukarabati huo. 
Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya CRDB Dk. Charles Kimei akipanda mti wa kumbukumbu wakati wa hafla ya kukabidhi wodi ya watoto katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro.
 Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid (katikati), akishiriki kufanya usafi katika jengo la wodi ya watoto katika hospitali ya Mkoa wa Morogoro ambayo imefanyiwa ukarabati mkubwa na benki ya CRDB. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo Dk. Charles Kimei akishiriki katika zoezi la kufanya usafi. Hafla hiyo ilifanyika mjini Morogoro juzi. Kulia ni Meya wa Manispaa ya Morogoro, Amir Nondo.
 Mkurugenzi wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akiteta jambo na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Steven Mashishanga.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad