HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, March 20, 2013

Watanzania rome washuhudia Baba Mtakatifu Francis akizindua Utume wake kwa Ibada Maalum

Siku ya Jumanne, tarehe 19 machi, majira ya saa tatu na nusu asubuhi, Baba Mtakatifu Francis, amezindua rasmi utume na utawala wake kwa Ibada ya Misa, katika Uwanja wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, mjini Vatican.

 kwenye Ibada hii ya uzinduzi Baba Mtakatifu ameongoza Ibada pamoja na Makardinali na Maaskofu wapatao 180 na kuhudhuriwa na Wakuu wa nchi 31, Viongozi wa Kifalme 6, Wana Wafalme 3, Mawaziri Wakuu 11. Ibada hii iliudhuliwa na umati wa watu, sio tu waumini wa Kikatoriki bali hata waumini wa madhehebu mbalimbali na zaidi watu tokea dini mbalimbali. Umati wa watu unakadiriwa kutokupungua 200.000. 

Katika Ibada hii, Baba Mtakatifu alivalishwa Pete ya Petro na Kardinali Angelo Sodano , ikiwa kama ishara ya wadhifa wake. 
Bendera ya Tanzania ilipeperushwa vizuri sana na umati mkubwa wa Watanzania walioudhulia Tukio ili la Kihistoria.

Kwa picha na video ya Tukio ili la Kihistoria mnakaribishwa kutembelea blog ya Jumuiya ya Watanzania Rome:www.watanzania-roma.blogspot.com

Picha zote zimeletwa kwenu na ndugu: Andrew Chole Mhella.

  
                                Baba Mtakatifu akipita kubariki watu 
              Bendera ya Tanzania ikipeperushwa mbele ya Baba Mtakatifu.
                                    Bendera yetu ikipepea katikati ya Umati wa Watu.
       Kulia ni katibu wa Jumuiya ya Watanzania Roma Ndugu 
Andrew Chole Mhella pamoja na Ndugu Safari Mwacha wakiipeperusha 
                                 bendera ya Tanzania.
              Masista na ma Padri wa Kitanzania wakiifurahia bendera yetu. 
                    Kwa pembeni ni baadhi ya Watalii wa kiargentina.
      Furaha ziliwajaa baadhi ya Watanzania waliokuwepo mbele ya Kanisa                                       Takatifu la Mtakatifu Petro.
Katibu wa Jumuiya ya Watanzania Roma ndugu Andrew Mhella Pamoja na Ndugu Safari Silvanus Mwacha na ndugu Dusten wakipata picha ya Pamoja na askali waliokuwepo kwenye kuhakikisha shughuli nzima inaenda salama.

1 comment:

  1. Sio Watanzania Wangekua watanzania wasinge geuza bendela

    ReplyDelete

Post Bottom Ad