Juu na chini ni Kaimu mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Utalii Tanzania ambaye pia ni Mkurugenzi wa Masoko wa Bodi hiyo Ndugu Devotha Mdachi akifungua Semina hiyo Maalum kwa Warembo wa Miss Utalii Tanzania 2012/13 .
Serikali
kupitia Bodi ya Taifa ya Utalii,imeendesha semina ya washiriki wa
Fainali za Taifa Miss Utalii Tanzania 2012/13 iliyo fanyika leo Katika
ukumbi wa mikutano uliopo Makao makuu ya Bodi ya utalii Tanzania.
Semina
hiyo ambayo ilifunguliwa na Kaimu mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Utalii
Tanzania ambaye pia ni Mkurugenzi wa Masoko wa Bodi hiyo Ndugu Devotha
Mdachi, imeandaliwa na Bodi ya Utalii kwa lengo la Kuwapiga msasa
washiriki hao kabla ya fainali ya Taifa itakayo fanyika 17.03.2013
katika ukumbi wa Dar Live.
Akifungua
Semina hiyo Ndugu Devotha mdachi pamoja na kuwakaribisha washiriki wote
makao makuu ya Bodi ya Utalii Tanzania aliwaasa washiriki hao kujifunza
na kuvielewa kwa kina vivutio vya utalii Tanzania ili wale watakao
shinda na kupata nafasi ya kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya
Dunia waweze kuitangaza vema Utalii wa Tanzania na nchi kwa Ujumla.
Aliwakumbusha pia wao kama warembo wa utalii wanalo jukumu la kuunda
mkono juhudi za Serikali kuhamasisha utalii wa Ndani lakini pia jukumu
la kutangaza vivutio vya utalii wa Tanzania kimataifa na Kimataifa.
Aliendelea kuwaasa pia wao kama warembo wa utalii wanapaswa kujivunia
utanzania na Maliasili zake huku wakidumisha Mila na Utamaduni wa
Tanzania na kwamba siku zote wanatakiwa kuwa na nidhamu ya hali ya juu
na mfano wa kuigwa katika jamii kwa maana warembo wa utalii ni alama ya
Urithi wa Taifa na kielelezo cha Mwanamke wa Kitanzania.
Aliwakumbusha
wale watakao shinda kwenda kutetea Mataji ya Dunia ambayo Miss Utalii
Tanzania wanashikiria .
Nae
mtoa mada Mkuu katika semina hiyo Ndugu Deogratias Malogo ambaye ni
Meneja wa Utafiti na Maendeleo wa Bodi ya Utalii Tanzania aliwafahimisha
warembo wa Miss Utalii Tanzania wa Fainali za Taifa 2012/13 kuwa secta
ya utalii ni secta muhimu katika Uchumi na kuchangia pato la Taifa kila
mwaka.
Alisema Secta ya utalii inachangia zaidi ya asilimia 20 ya pato
la Taifa kila mwaka na zaidi ya asilimia 25 ya pato la taifa la fedha za
kigeni kila Mwaka. Alisema Kidunia secta ya utalii inachangia zaidi ya
asilimia 12 ya ajira zote Duniani.
Warembo
hao walifundishwa Historia ya utalii Tanzania . Walifundishwa vivutio
vya utalii Tanzania, Mbinu za kutangaza utalii wa Tanzania Kitaifa na
Kimataifa, lakini aliwaelezea pia jitihada ambazo serikali kupitia bodi
ya taifa ya utalii na Mamlaka nyengine za utalii nchini imekuwa ikifanya
katika kukuza secta ya utalii na kutangaza vivutio vya utalii kitaifa
na Kimataifa.
Ndugu Malogo aliwaelezea juu ya umuhimu wa utalii wa ndani
katika kukuza na kuchangia pato la utalii la Taifa na kwamba wao kama
warembo wa utalii ni sehemu muhimu katika kukuza na kuendeleza secta ya
Utalii Tanzania kwani wao ni kioo cha jamii na mfano wa kuigwa kitabia
Mwenendo Muonekano na Hulka. Aliwatakia kila laheri wale watakao shinda
katika fainali hizo za Taifa kwenda kuwa mabarozi bora wa Tanzania
katika mashindano ya Dunia watakayo kwenda Kushiriki.
Nae
Rais wa Miss Utalii Tanzania alitoa shukurani na Pongezi kwa Bodi ya
Utalii Tanzania kwa juhudi kubwa wanazo fanya ya kuinua na kuendeleza
secta ya utalii nchini. Alipongeza na kushukuru pia hatua ya bodi ya
utalii, kwa kuendesha Semina Maalum kwa washiriki wa fainali za Taifa za
Miss Utalii Tanzania 2012/13 na kusema kwamba semina hii itakuwa ni
Dira na ufunguo kwa Miss Utalii Tanzania wa kutwaa mataji zaidi ya Dunia
katika mashindano yote watakayo shiriki na pia katika kutangaza na
kuhamasisha utalii wa ndani Kitaifa na Kimataifa.
Asanteni,
Fredy Tony Njeje
Marketing and Public Relation Miss Utalii Tanzania.
Raisi wa Miss Utalii Tanzania Organisation Ndugu Erasto G. Chipungahelo Akiishukuru Bodi ya Utalii Tanzania kwa Kubari kwao kufanya semina hiyo ya Mafunzo ya utalii kwa Warembo wa Miss Utalii Tanzania Taifa 2012/13.
Washiriki wa Miss Utalii Tanzania Taifa 2012/13 wakipitia kwa umakini majarida yanayo elezea Utalii Tanzania
Washiriki wa Miss Utalii Tanzania Taifa 2012/13 wakiwa katika picha ya pamoja na Baadhi ya viongozi pamoja na wafanyakazi wa Bodi ya Utalii Tanzania.
Washiriki wa Miss Utalii Taifa 2012/13 wakiwa katika picha ya pamoja Mara baada ya Semina Maalum ya Mafunzo kwisha.

No comments:
Post a Comment