HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, March 30, 2013

UPDATES: IDADI YA MAITI ZILIZOPATIKANA KATIKA AJALI YA KUPOROMOKA KWA JENGO JIJINI DAR YAFIKIA 24 USIKU HUU

Baadhi ya Magreda yaliopo kwenye eneo lililotokea janga la kuporomoka kwa jengo lenye urefu wa ghorofa 16,mtaa wa Indra ghand katikati ya jiji la Dar es Salaam,yakiendelea na kazi ya kuondoa kifusi cha jengo hilo ili kuweza kutoa miili ya watu waliopo chini ya kifusi hicho.ambapo usiku huu wameweza kutoa miili ya watu wanne na kufanya idadi kuwa ni watu ishirini na nne (24),kwani mpaka mchana wa leo walikuwa wameweza kutoa miili ishirini (20).zoezi la kutafuta miili mingine bado linaendelea hivi sasa.
 Baadhi askari wa Kikosi cha Zima moto kutoka Kampuni ya Ulinzi ya Night Support wakimwagia maji kifusi hilo ili kilainike na kufanya uraisi kwa Magreda kuweza kutoa udongo.
 Baadhi ya Mafundi wakiendelea na kazi ya kukata nondo zilizokuwepo kwenye jengo hilo ili kuwezesha urahisi wa kubeba.
 Baadi ya waokoani wakiangalia na kuelekezana namna watakavyoweza kuendelea na kazi yao ya uokoaji.
 Katika eneo hili ndiko kunaonekana kuna idadi kubwa ya watu,kwani harufu nzito inatokea katika eneo hili na kupelekea waokoaji kuweza kuondoa udongo kwa kutumia vifaa vya mikono kama waonekanavyo hapa.
 Vijiko vya Magreda vikiendelea kupunguza udongo kwa juu ili kuwarahisishia wanaotumia vifaa vya mikono.
  Kazi inaendelea.

1 comment:

  1. grader,wheel loader,excavator/digger. grader ni ile ya kutengeneza barabara yenye jembe katikati,excavator hizo pichani zenye mkono,wheel loader ni kijiko nayo iko pichani na bulldozer inayosukuma na kung,oa miti.sorry

    ReplyDelete

Post Bottom Ad