Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizindua shule mpya ya msingi ya Mabwepande jijini Dar es salaam,iliyojengwa kwa ufadhili wa kampuni ya Home Shopping Cenrre
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka sahihi kwenye kitabu cha wageni kabla ya kuzindua shule mpya ya msingi ya Mabwepande jijini Dar es salaam,iliyojengwa kwa ufadhili wa kampuni ya Home Shopping Cenrre
Rais Kikwete akimsikiliza Mkurugenzi wa Home Shopping Centre wakati akikabidhi shule hiyo
Rais Kikwete akimshukuru Mkurugenzi wa Home Shopping Centre kwa kujenga shule ya msingi Mabwepande yenye majengo na samani za kisasa. Picha na Raqey Mohamed
Rais Dkt.Jakaya akikagua nyumba za polisi katika eneo la Mabwepande zinazojengwa kwa msaada wa kampuni ya TSN ya jijini Dar es Salaam.Kushoto ni mkurugenzi mkuu wa Kampuni ya TSN Bwana Farough Ahmed Baghozah
|
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kuzindua kituo cha polisi Mabwepande huku Kamanda wa Polisi Kanda maalum Suleiman Kova akiangalia.Kituo hicho cha kisasa kimejengwa kwa msaada wa kampuni ya TSN.
Kamanda wa Polisi Kanda maalum ya Dar Es Salaam Suleiman Kova akimuongoza Rais Dkt. Jakaya Kikwete kukagua kituo kipya cha Polisi Mabwe Pande wilaya ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akitembelea Daraja la Suka Golani jijini Dar es Salaam.Kushoto kwake ni Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Mhe Yusuf Mwenda na mbunge wa Ubungo John Mnyika.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akifunua kitambaa kufungua rasmi Daraja la Suka Golani jijini Dar es Salaam.Kushoto anayeangalia ni mbunge wa Ubungo John Mnyika.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na baadhi ya wananchi waishio eneo la Golani Kimara Suka muda mfupi baada ya kuzindua Daraja la Suka Golani.
Wananchi wa vyama mbalimbali vya Siasa wakishangilia wakati Rais Jakaya Kikwete alipokuwa akiwahutubia muda mfupi baada ya kuzindua Daraja la Suka Golani jijini Dar es Salaam jana mchana
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kuzindua Daraja la Suka Golani jijini Dar es Salaam.Wengine katika picha kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam Bwana Madabida,Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Bwana Jordan Rugimbana,Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Bwana Sadik Meck Sadik,Meya wa Kinondoni Mstahiki Yusuf Mwenda na kushoto ni Mbunge wa Ubungo Mhe. John Mnyika.Picha na Ikulu.
No comments:
Post a Comment