Katika
kipindi cha Makutano kinachoendeshwa na Fina Mango wiki hii alifanya
mahojiano na Miss Tanzania na Miss World Africa 2005, Nancy Sumari
kuhusu mambo mbalimbali yanayomhusu katika maisha ya kabla na baada ya
kutwaa mataji hayo makubwa na kuingia katika historia kama Miss Tanzania
aliefanya vizuri zaidi kwenye mashindano ya ulimbwende duniani.
Nancy
ambaye hivi karibuni amezindua kitabu cha watoto alichokipa jina la
Nyota Yako alielezea nini hasa kilichomsukuma hadi kuamua kuandika
kitabu hicho na kusema ilitokana na baada ya kuwa mama na kujikuta kila
akienda maduka ya vitabu anakosa vitabu vya watoto vilivyoandikwa na
waandishi wa Tanzania na kukuta vingi ni kutoka nje ya nchi, hivyo
kuamua kuandika kitabu ambacho watoto wa kike wa Tanzania wataweza
kukisoma na kuvutiwa kufanya kile ambacho muandishi amekielezea. “Kwa
hivi sasa kitabu kinapatikana maduka ya Scholastica Mlinani City na pia
Novel Idea Masaki na Ohio kwa shilingi 5,000 tu” alisema Nancy.
Lakini
Nancy alikuwa na stori ya kusisimua kwani anasema kabla ya kuingia
kwenye mashindano ya urembo alilazimika kufanya kazi kama muuzaji katika
duka la fenicha kwa mshahara wa shilingi lakini moja na ishirini kwa
mwezi. Hii ilitokana na kukwama kupata nafasi ya kujiunga na Chuo Kikuu
cha Dar es Salaam, kitivo cha Sheria kutokana na chuo hicho kutoruhusu
mwanafunzi aliemaliza kidato cha nne kwa elimu ya Kenya kujiunga moja
kwa moja kwa ajili ya shahada.
Nancy
amesema alifanya kazi hiyo kwa moyo wote hadi alipopata nafasi ya
kushiriki taji la Miss Dar Indian Ocean baada ya kuonwa na wandaaji wa
shindano hilo na kuibuka mshindi wa pili na baadae kuibuka Miss
Kinondoni na hatimaye Miss Tanzania huku akisema kufanya kila kitu bila
kuogopa kushindwa ndio siri hasa ya kufanikiwa licha ya kutokuwa na
uzoefu wowote katika suala la urembo wa wakati huo na kusema hatimaye
alifanikiwa kupata nafasi ya kuingia chuo kikuu cha Dar es salaam na
atatarajia kumaliza masomo yake mwezi Julai.
Alipoulizwa
nini ushauri wake kwa vijana wanaochipukia alisema “Let’s all try to
become better people, everyone makes mistake no one is perfect lakini ni
muhimu kama binadamu kujitahidi kufanya vitu sahihi sawa na unapoona ua
linafifia linamwagilizie maji likue na unapomuona mwenzio anahitaji
msaada na unayo nafasi ya kumsaidia usisite”
Mahojiano yote yanapatikana katika:
Muendeshaji wa kipindi cha Makutano Fina Mango akimsikiliza Nancy Sumari
Nancy Sumari akijibu moja ya maswali aliyoulizwa na Fina Mango
No comments:
Post a Comment