Huyu ni binti ZAWADI KARIM (16), mkazi wa Mshindo,katika Manispaa ya Iringa ambaye amepigwa na kunyweshwa mkojo na mama yake mdogo aitwaye Ever Ubamba. Majirani wamesema kuwa vitu vilivyotumika kumwadhibu vilikuwa ni pamoja na nyaya za simu, mkanda na vipande vya chupa vilivyotumiwa kumchoma.
MKASA WA MPAKA KUFIKIA ADHABU HIYO UKO KAMA IFUATAVVYO
Zawadi ambaye kimsingi anaishi na mama yake mzazi ambaye kwa kipindi hicho dada mtu huyo alikuwa anaumwa. Ever alikuwa nje na marafiki zake ndipo mama yake mdogo huyo akamwita ndani ya nyumba yao hiyo wanayoishi mtaa wa mshindo
Baada ya kumwita na kisha mtoto huyo kushindwa kusikia baadaye aliitika na kuingia ndani ndipo alipo ambiwa avue nguo zote amri iliyotolewa na mama yake huyo mdodo Ever baada ya muda mfupi Zawadi alianza kupokea kipigo kikali kutoka kwa mama yake huyo mdogo.
Katika kipigo hicho Zawadi inadaiwa kwamba alipigwa pamoja na kunyweshwa mkojo kutoka kwa mama yake mdogo huyo.
Zawadi ambaye ni mtoto wa kuzaliwa na Dada yake Ever inadaiwa kipigo hicho kimesababishwa na tuhuma kwamba eti familia hiyo haina mtoto kama yeye.
Zawadi inadaiwa aliwahi kwenda Zanzibar kwa nia ya kufanya kazi na baada ya muda mama yake mzazi ambaye jina lake bado halijafahamika alimpigia simu arudi nyumbani na mara baada ya kurudi ndipo kutokuelewana huko kukajitokeza.
Inasimuliwa kuwa kisa cha yote hayo ni madai ya Zawadi kuomba aoneshwe Baba yake mzazi ili walau aweze kupata pumziko la adha anazozipata kutoka kwa ndugu zake.
Aidha, taarifa za ndani zinasema kuwa Mama yake Zawadi alimtupa akiwa mtoto mchanga na kuokotwa na wasamaria wema na kulelewa na Bibi yake ambaye kwa sasa amefariki dunia.
Watuhumiwa wa tukio hili, Mama mzazi pamoja na Mama mdogo, wanashikiliwa na jeshi la Polisi katika kitengo cha Dawati la Jinsia, kwa mahojiano zaidi.
Chanzo cha Habari hii ni kwenye blogu ya Francis Godwin.
Mwili wa Mtoto Zawadi ukiwa umedhuliwa vibaya.
No comments:
Post a Comment