Maandalizi
ya Mbio za Nyika za Kilimanjaro Maarufu kama Kilimanjaro Marathon 2013
yanafikia kiele hii leo na kesho ndio kivuvumbi na jasho wakati maelfu
ya wanariadha na watu wa kawaida wakitimua vumbi katika mbio hizo
zinazofanyika katiua mji wa Moshi mkoani Kilimanjaro.
Pichani ni baadhi ya wakimbiaji wakijiandikisha kwaajili ya kushiriki mbio hizo zitakazo fanyika Machi 3,2013 mjini Moshi na zitakuwa za makundi mbalimbali 42KM, 21KM na 5km Fun Run.
Makundi
mbalimbali katika Jamiui nayo yanashiriki ikiwa ni pamoja na walemavu
ambao pichani wakiwa katika banda la kujiandikishia.
Maofisa watakao simamia Mbio hizo Machi 3, 2013 wakiwa Uwanja wa Ushirika Mjini Moshi kuchukua vifaa.
Mbio za kujifurahisha kwa watoto na watu wazima zipo na hapa wakijiandikisha.
Baadhi ya wadhamini wakiwa tayari wamesha pamba mabanda yao ndani ya Uwanja wa Ushirika Mjini Moshi.
Mitaani napo Mabango ya Mbio hizo yamewekwa.Picha na Father Kibevu Blog
nimeshaanza matizi, mwakani nami nitashiriki! Tena nimekumbuka, Heri ya siku yako ya kuzaliwa @ Michuzi Jr.
ReplyDeleteMama Malaika
UK