HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, March 2, 2013

Heri ya Siku yetu ya Kuzaliwa Kina Sieeeeee

Othman Michuzi a.k.a Mzee wa Mtaa kwa Mtaa
 
Napenda Kuchukua Fursa hii Kumshukuru Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehma na Mwenye Kurehemu kwa kunijaalia Uhai na afya njema hadi kufikia siku hii ya leo,ambapo ninayo furaha kubwa sana kwa kuongeza namba moja katika umri wangu,kwani bila yeye hakuna kitu chochote kinachoweza kufanyika.

pia nitakuwa ni mchoyo wa Fadhila iwapo sitotoa shukrani za kipekee kwa ndugu zangu woote (wakiwepo wazazi) kwa kunilea na kukikuza katika makuzi yaliyo mema hadi leo hii kufikia hapa nilipo.

pia nawashukuru marafiki,jamaa zangu pamoja na Wadau woote popote pale mlipo ambao kwa namna moja ama nyingine mmekuwa ni mchango mkubwa katika maisha yangu na kunifanya kila siku niwe bize kuhakikisha libeneke halilali mpaka kieleweke.Nawashukuruni sana tena sana na Mungu awabariki nyoote.

Katika siku hii Muhimu,sipo peke yangu,kwani ni wengi pia tunasherehekea siku yetu ya kuzaliwa,wakiwemo wadau hawa wanaoonekana kwenye picha hizo hapo chini.

SASA TUNAZISUBIRIA HIZO ZAWADI ZETU KWA HAMU.
Mdau Dj LUKE Mzee wa Vijimambo Blog.
Khalifa Ilunga a.k.a CPWAA.
Farha Sultan.

1 comment:

  1. Heri ya siku ya kuzaliwa. Nimeku-miss sana, wadogo zako Malaika & Denzil wanakutakia uwe na maisha marefu yenye amani na furaha. Walikuja bongo wakakukosa.

    Mama malaika

    ReplyDelete

Post Bottom Ad