UONGOZI wa Bendi ya Mashujaa Wana Kibega,
umesema uvumi wa kuwa Wanamuziki Charles
Gabriel 'Chalz Baba' na Sudi Mohamed MCD
wanatimka katika bendi hiyo si kweli.
Akizungumza jijini Dar es Salaam leo Mkurugenzi wa
bendi hiyo Sakina Mbange, amesema kuwa kupanda
kwa wanamuziki hao katika jukwaa la bendi
nyingine si kama wamehamia huko.
Mbange alisema kuwa kila mtu ana tambua maana
ya sheria ambapo mikataba ya hao wanamuziki ipo
kisheria hivyo ni mali yao kwa sababu wana
mikataba.
"Nina amini kila mtu anatambua nini mana ya
sheria wanamuziki wetu wapo kisheria tumewapa
mikataba hivyo kama kuna mtu anajaribu
kuwashawishi atapata tatizo kubwa"alisema
Mbange.
Pia alisema wao hawawezi kumzuia mwanamuziki
kupanda jukwaani hivyo wana amini kila bendi ni
kama ndugu.
Mbange alisema wanamuziki hao wapo kazini kama
kawaida na wanaendelea na kazi zao za kila siku.
Nae Mwamuzi Chalz Baba amewataka mashabiki wa
bendi yake wasiwe na shaka na tetesi zilizozagaa
kuwa yuko mbioni kutimka na kuamia bendi yake ya
zamani ya The African Stars Twanga Pepeta.
Alisema si kweli kama anajiandaa kurejea Twanga
Pepeta, alisema ni uvumi tu ambao kuna watu
wameamua kuutengeneza.
"Kwanza sina mpango wa kuondoka sehemu
ambayo nina amini nipo vizuri kikazi na
ninashirikiana na wenzangu kwa moyo mmoja...na
nafanya kazi kwa mkataba"alisema Chalz Baba.
Alisema kuna watu wameamua kueneza uvumi huo,
wana ajenda ya kuvuruga mshikamano uliopo ndani
ya Mashujaa.
“Mimi ni mwanamuziki wa Mashujaa, nina mkataba
mrefu na nina uheshimu, bendi yoyote inayonihitaji
ni lazima ikae mezani na Mashujaa hakuna njia ya
mkato nina amani na maisha ya Mashujaa, natarajia
kukaa hapa hadi mwisho wa mkataba wangu”
alisema Chaz Baba.
Akifafanua kuhusu kupanda jukwaa la Twanga
Pepeta jambo ambalo limezidi kupalilia uvumi wa
kuondoka kwake Mashujaa, Chalz Baba alisema
kukwea jukwaa la Twanga au bendi nyingine yoyote
ni sehemu ya kukaribisha urafiki baina ya bendi yake
na bendi zingine. “Hii tunaita kusalimiana kisanii, ni
jambo la kawaida sana” alifafanua
No comments:
Post a Comment