HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, March 19, 2013

Benki ya Posta Tanzania yatoa mchango wake kwa shughuli ya utoaji tuzo kwa waandishi bora wa habari nchini

Benki ya Posta Tanzania imetoa mchango wa shilingi milioni 1.5 kwa Baraza la Habari Tanzania (MCT) kwa ajili ya shughuli ya kutoa tuzo kwa waandishi wa habari (Excellence in Journalism Awards). 

Shughuli za kutoa tuzo hizo zinatarajiwa kufanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee tarehe 5 Aprili, na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Raisi wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi Alli Mohammed Shein.

 Akiongea kwenye sherehe fupi ya kukabidhi msaada huo liliyofanyika kwenye makao makuu ya benki hiyo, Meneja Mahusiano Mwandamizi wa benki ya Posta Noves Moses amesema benki hiyo inatambua umuhimu wa kazi zinazofanywa na waandishi wa habari katika kuelimisha jamii juu ya masuala mbalimbali ya muhimu kwa mstakabali wa maisha yao.

 Benki hiyo imedhamini kitengo cha Uchumi na Biashara, kwa kuelewa umuhimu kwa habari za biashara kwa manufaa ya watanzania na uchumi wa nchi kwa ujumla. Akipokea msaada huo,Afisa Programu,Udhibiti na Viwango wa baraza la habari Tanzania Paul Mallimbo, ameishukuru benki ya Posta kwa mchango wake kwenye shughuli hiyo ya muhimu, na ametoa wito kwa taasisi nyingine kuiga mfano wa benki hiyo ya kuwatambua waandishi bora na kuwatuza, ili kuwapa moyo waendeelee kufanya kazi nzuri zinazokubalika. 
Meneja mahusiano mwandamizi wa Benki ya Posta Noves Moses (kushoto) akikabdhi hundi ya shilingi milioni moja na nusu kwa Afisa Programu wa MCT,Paul Mallimbo kwa ajili ya kuchangia shindalo la muandishi bora, kwenye sherehe fupi iliyofanyika makao makuu ya benki hiyo.
Meneja mahusiano mwandamizi wa Benki ya Posta Noves Moses akizungumza na waandishi wa habari.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad