Urban Pulse Creative inakuletea picha ya ziara ya Mh waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo alipotembelea makao makuu kampuni ya BG Group inayofanya kazi ya uchimbaji wa gesi na mafuta ili kuangalia ufanisi wake na jinsi gani itakavyoweza kutunufaisha sisi watanzania kama ikipewa fursa ya kuwekeza nchini kwetu.
BG group ni mojawapo ya kampuni kubwa duniani inayoongoza katika uchimbaji, utunzaji, usambazaji wa gesi asilia.Tangu kuanzishwa kwake mwaka 1996 BG Group imeweza kujiimarisha zaidi kwa kujijengea uzoefu mkubwa na historia nzuri katika sekta hii nyeti ya nishati. Pamoja na kuwa makao yake makuu yakiwa mjini Reading nchini Uingereza vilevile kampuni hii ishafanya kazi katika nchi ishirini duniani ndani ya mabara matano tofauti ikiwa na wafanyakazi zaidi ya elfu sita kutoka mataifa mbalimbali duniani.
Katika ziara hii Mh waziri Muhungo aliambatana na Mh Balozi wetu Peter Kallaghe, Mr Sosthenes Masau Bigambo Massola, Dr Athanas Simon Macheyeki (Geological Survey Tanzania), Mr Seleman Hatibu Chombo ( Idara ya Nishati na Madini Tanzania) na Mr Bikash Dawahoo mwakilishi kutoka Ubalozi wa Uingereza Tanzania

Makao makuu ya Kampuni ya BG
Mh Waziri Profesa Muhongo akipokea maelezo kutoka kwa injinia wa BG Group
Control room ya BG Group
Mh Waziri akifuatilia maelezo kutoka kwa msemaji wa kampuni ya BG ambapo ramani inaonesha live shughuli zainazoendelea katika visima vya gesi inayochimba nchini Tanzania
Mh Waziri akitembelea makao makuu ya BG Group
Mh waziri Muhongo akisalimia na CEO wa BG Chris.
Mh waziri Muhongo akisalimia na CEO wa BG Chris katika picha ya pamoja na ujumbe wake na wa kampuni hiyo
No comments:
Post a Comment