Meneja
wa Mpango wa Taifa wa Damu NBTS, Dk. Efesper Nkya akimkabidhi cheti cha
kushukuru mchango wa Tigo kuchangia damu mkoa wa Lindi mwaka jana kwa
Mkurugenzi Mkuu wa Tigo Tanzania Diego Gutierrez kulia ni Afisa wa Ushirika wa Jamii wa Tigo Bi. Woinde Shisae.
---
Tigo
Tanzania leo imekabidhiwa cheti cha shukrani kutoka kwa Mpango wa Taifa
wa Damu Salama kwa msaada wake mkubwa wa kuhamasisha umma juu ya
umuhimu wa kuchangia damu kupitia mpango wa kuchangia damu salama ambao
ulifanyika katika mkoa wa Lindi mwezi mwaka jana.
Mpango
huu ulifanyika katika mkoa wa Lindi Uwanja wa ILULU, na ulianza tarehe
25 Novemba 2012 na ulihitimishwa Desemba 1, 2012 kuashiria siku ya
Ukimwi Duniani. Lengo kuu la zoezi hilo lilikuwa kuwaalika na
kuhamasisha wachangiaji wa damu kwa njia ya hiari, pamoja na kutoa fursa
kwa wanajumuia kupima VVU na kuelimishwa bure juu ya umuhimu wa tabia
hatarishi za maambukizi ya VVU.
Mpango
huu ulikuwa na mafanikio makubwa kwani zaidi ya uniti 300 za damu
zilikusanywa kutoka kwa wale ambao walishiriki. Maadhimisho ya mpango
huo yaliongozwa na mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Dr Jakaya Mrisho Kikwete, ambaye alikuwa mgeni rasmi katika Siku ya
Ukimwi duniani iliyofanyika mkoa wa Lindi mwaka jana.
Mpango
huo ulifanikiwa kuwaelimisha wanajamii juu ya umuhimu wa kuchangia damu
na jinsi zoezi rahisi kama hili linaweza kuokoa maisha ya mwanadamu,
kwa kupunguza vifo vya uzazi, watoto wachanga, na mama wajawazito kwa
kiwango cha asilimia 80% kati ya wapokeaji damu.
"Sisi
kama Mpango wa Taifa wa Damu Salama tunapenda kuchukua fursa hii kutoa
shukrani zetu kwa Tigo Tanzania kwa msaada wao mkubwa katika programu
hii na imeonyesha kwamba wao wana moyo wa kuwasaidia Watanzania
kuhakikisha wanaishi maisha bora na afya njema", alisema Dk Efesper
Nkya, Meneja wa Programu NBTS wakati akikabidhi cheti.
Mkurugenzi
Mkuu wa Tigo Bwana Diego Gutierrez alisema akipokea cheti kuwa “kama
Tigo tunajisikia heshima na fahari kubwa kuwa sehemu ya mpango huu wa
kuhamasisha umma juu ya umuhimu wa mchango wa damu salama, na tunafurahi
kuwachangia Watanzania ili waishi maisha bora na afya njema. Ni furaha
kubwa kwangu mimi kukubali hati ya shukrani kwa niaba ya Tigo Tanzania
na napenda kuchukua fursa hii kushauri na kuwahamasisha Watanzania wote
kuchangia damu salama, kwani mchango wao unaweza kuwa sababu kubwa
katika kuokoa maisha ya mwanadamu mwingine ".

No comments:
Post a Comment