NA HAMZA TEMBA - OFISI YA MKUU WA MKOA RUKWA
Mwenyekiti wa chama watu wenye ulemavu wa ngozi Tanzania "Tanzania Albino Society" (TAS) ndugu Ernest Kimaya ameiomba serikali kupitia upya sheria ya haki ya kuishi kwa kuwapatia adhabu kali ya kifo wale wote wanaohusika kwa vitendo vya kinyama dhidi ya albino ikiwepo mauaji na ukataji wa viungo vyao wakiwa hai kwa kile kinachoaminika katika imani za kishirikina kuwa ni kujipatia utajiri.
Aliyasema hayo jana akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya ofisini kwake alipomtembelea akiongozana na viongozi wengine wa chama hicho kumpa pongezi zake za dhati kwa kile alichosema ni mfano wa kuigwa kwani tangu vitendo hivyo vianze hapa nchini kwa muda wa miaka mitano iliyopita ni Mkoa wa Rukwa pekee umefanikiwa kuwakamata wahalifu wa namna hiyo pamoja na kiungo husika kwa muda mfupi usiozidi siku tatu.
Amesema kuwa maalbino wamenyanyasika sana katika nchi yao kwa kukosa uhuru na amani kama watu wengine jambo ambalo ni kinyume na haki za binadam. "Watu waliokamatwa sio wa kuachiwa huru, wabanwe hata kuchomwa moto wataje wahusika wengine kwani mtandao wao ni mmoja na inatia uchungu sana kwa sisi maalbino" alisema mwenyekiti huyo.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Rukwa alimshukuru mwenyekiti wa chama hicho na viongozi wenzake kwa kufika Mkoani kwake kujionea hali halisi baada ya kuskika kwa matukio hayo ya kinyama kwa Albino wenzao na pia kuwashukuru wananchi na jeshi la Polisi kwa ushirikiano mzuri walioutoa kufanikisha watuhumiwa kutiwa mbaroni ili haki iweze kutendeka. Mkuu huyo wa Mkoa alisema vitendo kama hivo kaamwe havitaweza kuvumilika Mkoani kwake.
Kumekuwepo na matukio ya kusikitisha hivi karibuni ya ukatili kwa Albino ambapo mama mlemavu wa ngozi Maria Chambanenge (39) mkazi wa kijiji cha kavifuli katika Wilaya ya Sumbawanga alivamiwa nyumbani kwake usiku wa manane na kukatwa mkono wake wa kushoto na watuhumiwa ambao wameshakamatwa na jeshi la polisi na taratibu za mashitaka yao zinaendelea.
Vilevile katika bonde la ziwa Rukwa kata ya Milepa mtoto wa kiume mwenye ulemavu wa ngozi ‘albino” Mwigulu Matomange Magessa mwenye umri wa miaka saba ameshambuliwa na vijana watatu waliovaa kininja na kumkata mkono wake mmoja na kutokomea na kusikojulikana. Polisi wanaendelea na uchunguzi kuwabaini wahusika.
Matukio yote hayo yanahusishwa na wahalifu kutoka Mkoa jirani wa Mbeya ambapo vitendo hivi vya imani za kishirikina vimeshamiri.
Mwenyekiti
wa chama cha watu wenye ulemavu Tanzania (TAS) "Tanzania Albino
Society" ndugu Ernest Kimaya akizungumza kwa uchungu mbele ya Mkuu wa
Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya (Pichani chini) kuelezea juu ya
tukio la kinyama alilofanyiwa Maria Chambanenge (39) la kukatwa mkono
wake wa kushoto kwa kile kinachodaiwa kwa imani za kishirikina kuwa ni
kupata utajiri. Watuhumiwa waliohusika na tukio hilo ambao pia yupo mume
wake na muathirika wameshakamatwa na polisi na kuonyesha mkono huo,
taratibu za mashitaka zinaendelea ili haki iweze kupatikana. Mwenyekiti
huyo ameiomba Serikali kufkiria adhabu kali kwa watuhumiwa kama ho
ikiwepo kunyongwa ili fundisho kwa wengine na Albino waweze kuishi
katika nchi yao kwa amani.
Mwenyekiti wa TAS akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa ofisini kwake. Kulia ni Katibu Mkuu wa chama hicho ndugu Mohammed Chanzi.
Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akizungumza kwa uchungu na
kutoa onyo kali kuwa vitendo hivyo vya kinyama havitavumiliwa. Alitoa
wito kwa wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kutokomeza vitendo hivyo.
Kabla ya kwenda kumtembelea mgongwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa aliandaa chakula kwa wageni wake.
Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya na msafara wake pamoja na
viongozi wa chama cha Albino Tanzania (TAS) wakimfariji Mama Maria
Chambanenge walipomtembelea katika hospitali kuu ya Mkoa Rukwa ambapo
hali yake kwa sasa inaendelea vizuri japo ameongezewa ulemavu mwingine
wa viungo kwa kukatwa mkono wake wa kushoto.
Mwenyekiti
wa chama cha watu wenye ulemavu Tanzania (Albino) ndugu Ernest Kimaya
akimfariji Mama Maria Chambanenge ambaye anaendelea kupatiwa matibabu
katika hospitali kuu ya Mkoa Rukwa kufuatia kukatwa mkono wake wa
kushoto na watu walioshirikiana na mume wake na ambao tayari wapo
mikononi mwa polisi.







No comments:
Post a Comment