Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitoa mkono wa pole na kuwafariji ndugu, jamaa na marafiki wa familia zilizoondokewa na watoto na wazazi wao kufuatia ajali ya barabarani iliyotokea maeneo ya kijiji cha Kibiki, Ubena Zomozi katika mkoa wa Pwani Februari 11, 2013 iliyoua hapohapo watu wanane wakiwemo wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Chalinze baada ya gari dogo aina ya Toyota Mark II lililokuwa limebeba abiria wanane kugongana uso kwa uso na roli.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifariji ndugu, jamaa na marafiki wa familia zilizoondokewa na watoto na wazazi wao kufuatia ajali ya barabarani iliyotokea maeneo ya kijiji cha Kibiki, Ubena Zomozi katika mkoa wa Pwani Februari 11, 2013 iliyoua hapohapo watu wanane wakiwemo wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Chalinze baada ya gari dogo aina ya Toyota Mark II lililokuwa limebeba abiria wanane kugongana uso kwa uso na roli.
Rais
Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia moja ya picha za ajali hiyo
alizopewa na wanafamilia walioondokewa na watoto na wazazi wao kufuatia
ajali ya barabarani iliyotokea maeneo ya kijiji cha Kibiki, Ubena Zomozi
katika mkoa wa Pwani Februari 11, 2013 iliyoua hapohapo watu wanane
wakiwemo wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Chalinze baada ya gari dogo
aina ya Toyota Mark II lililokuwa limebeba abiria wanane kugongana uso
kwa uso na roli.
Haya ndio magari yaliyopata ajali hiyo na kupelekea vifo vya watu wanane wakiwemo wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Chalinze.PICHA NA IKULU.
==== ====
Rais Jakaya Mrisho Kikwete Jumamosi hii ya Februari 16, 2015 amekwenda
kuhani na kufariji ndugu, jamaa na marafiki wa familia zilizoondokewa na
watoto na wazazi kufuatia ajali ya barabarani maeneo ya kijiji cha
Kibiki, Ubena Zomozi katika mkoa wa Pwani iliyotokea Februari 11, 2013
na kupoteza hapohapo maisha ya watu nane wakiwemo wanafunzi wa Shule ya
Sekondari ya Chalinze baada ya gari dogo aina ya Toyota Mark II
lililokuwa limebeba abiria wanane kugongana uso kwa uso na roli la
mizigo.
Familia
alizokwenda kuhani na kuzifariji ni pamoja na za marehemu Hassan Erasto
Kurunge (57), Maria Sadiki ((52) na mtoto wa mwaka mmoja Samweli Ismail
wa kata ya Ubena.
Wengie ni marehemu Essau Enos Mwamgingo (16) , Stella Isaack Kazimoto (18), Bahati George Mbena (17) na Latifa Maneno (17).
Akiwa
ameongozana na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe Mwantumu Mahiza na Mkuu wa
Wilaya ya Bagamoyo Mhe. Ahmed Kipozi, Rais Kikwete alieleza kusikitishwa
kwake kwa ajali hiyo, na kuwataka madereva wawe makini katika
kuzingatia sheria za usalama barabarani.
Rais
Kikwete alisikitishwa zaidi kwa taarifa kwamba gari hilo dogo lilikuwa
limebeba abiria wanane, na kuwa dereva wake ambaye pia alipoteza maisha,
hakuwa makini katika kuzingatia sheria za usalama barabarani.







No comments:
Post a Comment