HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, February 3, 2013

Rais Kikwete aongoza Sherehe za Maadhimisho ya Miaka 36 ya CCM mkoani Kigoma leo

 Mwenyekiti wa CCM,Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisisitiza jambo wakati wa hotuba yake kwa wananchi wa Mkoa wa Kigoma waliohudhulia Maadhimisho ya Miaka 36 ya kuzaliwa kwa CCM,yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika,Mkoani Kigoma jioni hii.
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndg. Abdulrahman Kinana akisema machache,muda mfupi kabla ya kumkaribisha Mwenyekiti wa CCM,Rais Jakaya Mrisho Kikwete (hayupo pichani} kuwahutubia wananchi wa Mkoa wa Kigoma jioni hii.
Waziri wa Uchukuzi,Dkt. Harisson Mwakyembe akiwahutubia wananchi wa Mkoa wa Kigoma jioni hii na kuwahakikishia kuwa sasa hivi mkoa wa Kigoma mambo yako vyema kabisa na treni itaendelea kufanyaka kazi kama zamani.
Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi CCM,Nape Nnauye akiongoza shughuli hiyo.

 Mwenyekiti wa CCM,Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwasalimia wananchi wa Mkoa wa Kigoma,wakati akiwasili kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika,kuongoza Maadhimisho ya 36 ya kuzaliwa kwa CCM,Mkoani Kigoma leo.
Mwenyekiti wa CCM,Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifurahia burudani ya ngoma. 
Chipkizi wa CCM Mkoa wa Kigoma wakifanya Gwaride la heshima kwa Mwenyekiti wa CCM,Rais Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa sherehe za Maadhimisho ya Miaka 36 ya kuzaliwa kwa CCM,yaliyofanyika jioni hii kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika Mkoani Kigoma.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad