Msimamizi wa Kiwanda cha Kuzalisha Nyuzi za Mkonge cha Gereza Kihonda lililopo mkoani Morogoro, Fidelis Muhaya akimuonyesha majani ya mkonge ambayo yamevunwa, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Malimi Malemi (Kushoto). Katikati ni Mshauri wa Masuala ya Jinsia wa Programu ya Sekta ya Sheria nchini, Wanyenda Kutta.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Malimi Malemi (wa pili kutoka kushoto) akiangalia nyuzi za mkonge ambazo zimeanikwa kwa ajili ya kukaushwa maji kabla ya kuingizwa kiwandani kwa ajili ya kuzilainisha na kuzisafisha. Kulia ni Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini, Kamishna Jenerali John Minja.
Naibu
Katibu Mkuu, Mwamini Malemi (wa pili kutoka kushoto) na Mkuu wa Jeshi
la Magereza nchini, Kamishna Jenerali John Minja (kulia) pamoja na
wageni waliotembelea kiwanda hicho wakiangalia mashine ya kubana mkonge
kwa ajili ya kupunguza ukubwa kabla ya kusafirishwa.
Naibu
Katibu Mkuu, Mwamini Malemi (katikati) na Mkuu wa Jeshi la Magereza
nchini, Kamishna Jenerali John Minja (kushoto) pamoja na wageni wengine
wakionyeshwa pamoja na kufafanuliwa zaidi na Msimamizi wa kiwanda hicho
Fidelis Muhaya jinsi inavyofanya kazi mashine ya kubana mkonge kwa ajili
ya kupunguzwa ukubwa.
Naibu
Katibu Mkuu, Mwamini Malemi (katikati) akizishika nyuzi za mkonge
zilizokamilika ambazo zipo tayari kwa ajili ya matumizi mbalimbali
nchini.
PICHA ZOTE NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI.

No comments:
Post a Comment