Mlango wa kuingilia maonyesho umeshatayarisha
Anna Lukindo(Anna Luks) akiwa kazini kutayarisha ufunguzi huu
Moja ya matumizi mbalimbali ya kanga kama mto katika kochi
Matayarisho yamepamba Ubalozi Tanzania nchini Uingereza.
Na Freddy Macha
Maonyesho
maarufu ya mavazi ya kimataifa –London Fashion Week- yatamega kitengo
chake cha kimataifa kusaidia kutangaza kazi za washoni wapya toka
Tanzania ndani ya Ubalozi wetu leo Ijumaa mjini London.
Mada
ya maonyesho haya yatakayoendelea kwa juma zima ni “Swahili Flavour”
(Ladha ya Kiswahili). Yategemea kutukuza kazi za Watanzania kupitia
wabunifu mavazi Christine Mhando (anayetumia jina la ubunifu: “Chichia
London”) na Anna Lukindo ( “Anna Luks”).
Christine
Mhando alihitimu chuo cha Usanii cha Kent mwaka 2002 na huhimiza mtindo
wa Kanga kama wajihi wa kazi zake, ilhali Anna Luks aliyemaliza chuo
cha Middlesex, London hutumia fani inayosisitiza kamba kamba, mavazi ya
kike kwa dunia ya kisasa. Wote wanasema wana lengo la kukuuza sanaa na
ubunifu, utamaduni wa Kitanzania, kutangaza taswira za Kiswahili na sura
mbalimbali za Afrika Mashariki. Pamoja nao wasanii hawa ni msaidizi
wao–ambaye bado anasomea upambaji mavazi, Margaret Waiyego - mzawa wa
Kenya.
Kaimu
Balozi wa Tanzania, Mheshimiwa Chabaka Kilumanga alisema jana kwamba
maonyesho haya ya kimataifa yatakua nafasi kubwa kwa Tanzania kujenga
jina lake na ni sehemu mahsusi ya kujivunia utamaduni wetu. Shirika la
maendeleo ya utamaduni na elimu British Council ndiye mgharamiaji wa
shughuli hii yenye lengo la kujenga vipaji na kazi za mavazi za washoni
wasiofahamika duniani.






No comments:
Post a Comment