HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, February 25, 2013

Katibu Mkuu Kiongozi,Balozi Ombeni Sefue atembele Benki ya Posta jijini Dar leo

 Katibu Mkuu Kiongozi,Balozi Ombeni Sefue (wa tatu kulia) akisikiliza maelezo Kibenki kutoka kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania,Sabasaba Moshingi (kulia) wakati wa ziara ya Balozi Sefue kutembelea Matawi ya Benki ya Posta ya Jijini Dar es Salaam leo,ambapo ametembelea Matawi ya Kariakoo,Mkwepu na Makao Makuu ya Benki ya Posta.
 Katibu Mkuu Kiongozi,Balozi Ombeni Sefue akisalimiana na baadhi ya maafisa wa Benki ya Posta wakati alipokuwa akiwasili kwenye Makao Makuu ya Benki ya Posta Tanzania,yaliopo mtaa wa Samora jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Kiongozi,Balozi Ombeni Sefue akizungumza na Wakurugenzi wa Benki ya Posta Tanzania katika makao makuu ya Benki hiyo yaliopo mtaa wa Samora jijini Dar es Salaam,mara baada ya kufanya ziara ya kutembelea matawi ya Benki hiyo jijini Dar es Salaam leo.
 Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania,Sabasaba Moshingi (pili kulia) akitoa ufafanuzi wa maswala ya utendaji wa Benki hiyo,kwa Katibu Mkuu Kiongozi,Balozi Ombeni Sefue (kulia) wakati wa Kikao na Wakurugenzi wa Benki hiyo,leo jijini Dar es Salaam.
 Meneja wa Benki ya Posta Tanzania Tawi la Mkwepu jijini Dar es Salaam,Ayub Sapi Mkwawa (kushoto) akisalimia na Katibu Mkuu Kiongozi,Balozi Ombeni Sefue ( wa pili kulia) wakati alipowasili kwenye tawi hilo leo.kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania,Sabasaba Moshingi.
 Meneja wa Benki ya Posta Tanzania Tawi la Mkwepu jijini Dar es Salaam,Ayub Sapi Mkwawa (kulia) akimuonyesha kitu Katibu Mkuu Kiongozi,Balozi Ombeni Sefue wakati akimfungulia Akaunti katika Tawi hilo.
 Katibu Mkuu Kiongozi,Balozi Ombeni Sefue akijaza fomu za kufungua akaunti katika Benki ya Posta Tanzania Tawi la Mkwepu jijini Dar es Salaam.
 Katibu Mkuu Kiongozi,Balozi Ombeni Sefue akibofya mashine maalum ya kutambua akaunti ya mteja.
 Katibu Mkuu Kiongozi,Balozi Ombeni Sefue akisikiliza maenezo kutoka kwa Mtoa huduma wa Benki ya Posta Tanzania Tawi la Mkwepu jijini Dar es Salaam.
 Chumba maalum cha kutolea huduma kwa wateja wanaopiga simu.
Mkurugenzi wa Uendeshaji na Teknohama wa Benki ya Benki ya Posta Tanzania,Jema Msuya (kushoto) akifafanua jambo kwa Katibu Mkuu Kiongozi,Balozi Ombeni Sefue wakati alipotembelea Tawi la Mkwepu jijini Dar es Salaam leo.
Katibu Mkuu Kiongozi,Balozi Ombeni Sefue (katikati walio keti) akiwa katika picha ya pamoja na Wakurugenzi wa Benki ya Posta Tanzania.
Wakurugenzi wa Benki ya Posta Tanzania wakiwa kwenye picha ya pamoja.

1 comment:

  1. nice! I real like the bank, HONGERA TPB kwa kuboresha huduma zenu.... kazeni buti

    ReplyDelete

Post Bottom Ad