Mkurugenzi wa Bendi ya Kalunde,Deo Mwanambilimbi (kati) akiimba huku wacheza shoo wa bendi hiyo Kushoto ni Queen Vero na kulia ni Frola Bamboocha wakiwa sambamba nae wakati wa onesho la Valentine lililofanyika kwenye ukumbi wa Trinit Oysterbay jijini Dar es salaam usiku wa kuamkia leo, Katika Onesho hilo pia bendi ya Kalunde imesherehekea kutimiza miaka 7 toka ianzishwe.
Mkurugenzi wa bendi ya Kalunde,Deo Mwanambilimbi (kushoto) Debora Nyangi Meneja wa bendi hiyo pamoja na Mwapwani mwimbaji wa bendi ya Kalunde kwa pamoja wakikata keki kuashiria sherehe za kutimiza miaka saba toka bendi hiyo ianzishwe.
Meneja wa Bendi la Kalude,Debora Nyangi akimlisha keki Mkurugenzi wa bendi hiyo,Deo Mwanambilimbi katika onesho la Valentine na sherehe za utimiza miaka 7 ya kuanzishwa kwa bendi hiyo.
Bendi la Kalude katika onesho la Valentine na sherehe za kutimiza miaka 7 ya kuanzishwa kwa bendi hiyo.
Mkurugenzi wa bendi ya Kalunde,Deo Mwanambilimbi akiwa katika picha ya pamoja na Debora Nyangi ambaye pia ni Meneja wa bendi ya Kalunde na pia wakiwa wanamuziki waanzilishi wa bendi hiyo.
Mashabiki wa bendi ya Kalunde wakijimwaga stejini wakati bendi hiyo ikitumbuiza kwenye ukumbi wa Trinit Oysterbay jijini Dar es salaam usiku huu.




No comments:
Post a Comment