HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, February 11, 2013

Dkt Shein katika maulid Tumbatu, Jongowe

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein akikata utepe kufungua zawia ya Tumbatu Jongowe,alipohudhuria katika maulidi ya Mtume Muhamad (SAW)
yanayosomwa kila mwaka katika kijijini hapo
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,(kushoto)  akitia ubani kuyafungua Maulid ya Mtume Muhammad (SAW) yaliyofanyika jana  Tumbatu Jongowe,alipohudhuria akiwa mgeni rasmi,(kulia) Kadhi Mkuu Sheikh Khamis Haji
  Mwanafunzi Mhadi Haji Vuai, wa madrasa Nurmunawar ya Tumbatu Jongowe akisoma maulid ya Mtume Muhammad (SAW) mlango wa kwanza
 Wanafunzi wa madrasatul Maamur ya Tumbatu Jongowe wakisoma Qaswida wakati wa maulid ya Mtume Muhammad (SAW)
 Baadhi ya Akina Mama wa Tumbatu Jongowe na Vijiji Jirani walioalikwa katika maulidi ya Mtume Muhammad (SAW) wakiwa nje ya zawia  ya kijijini hapo palipofanyika Maulid hayo
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,(wa pili kushoto)  akitiliwa marashi wakati wa kumswalia Mtume Muhammad (SAW),yalipofanyika Maulid huko  Tumbatu
Jongowe j
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,akipokea zawadi maalum kutoka kwa mwanafunzi Mohamed Haji Mohamed,iliyotayarishwa na wazee wa Tumbatu
Jongowe wakati wa Maulid ya Mtume Muhammad (SAW),
Baadhi ya waumini wa Dini ya Kiislamu wa Tumbatu Jongowe na Vijiji Jirani walioalikwa katika maulidi ya Mtume Muhammad (SAW) wakiwa katika zawia ya  kijijini hapo palipofanyika Maulid hayo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad