HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, February 12, 2013

CCM yapata Wajumbe 14 wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu Taifa mjini Dodoma

Mwenyekiti wa CCM,Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipigira kura kuchagua wajumbe wa Kamati kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa katika ukumbi wa White House uliopo makao makuu ya CCM mjini Dodoma jana jioni.Kushoto ni Makamu wa Mwenyekiti CCM Zanzibar Dkt.Ali Mohamed Shein, Wapili kulia ni Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana na Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM -Bara,Ndugu Philip Mangula.
Baadhi ya wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa wakipiga kura zao kuwachagua wajumbe wa Kamati kuu jana jioni mjini Dodoma katika ukumbi wa White House(picha na Freddy Maro).
Makatibu wa NEC, Zakia Meghji (Uchumi na Fedha) na Dk. Asha-Rose Migiro (Siasa na Uhusiano wa Kimataifa) wakipiga kura, wakati wa uchaguzi wa Wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM uliofanywa na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM jana jioni,wakati wa Kikao cha NEC kilichofanyika katika ukumbi wa White House, Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma. Kushoto ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye (Picha na Bashir Nkoromo).

 Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi katika kikao chake cha siku mbili Februari 10 na 11, 2013 kilichofanyika mjini Dodoma, pamoja na mambo mengine kimeridhia uteuzi na kufanya uchaguzi wa Wajumbe 14 wa Kamati Kuu yake.

Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM imeridhia uteuzi wa Dokta Salim Ahmed Salim kuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu kupitia nafasi 10 za uteuzi wa Mwenyekiti wa CCM. 

Wajumbe 14 waliochaguliwa kuwa wajumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ni:-

Wajumbe wa Kamati Kuu - Bara
1. Ndugu Pindi Chana

2. Ndugu Adam Kimbisa
3. Ndugu William Lukuvi
4. Dokta Emmanuel Nchimbi
5. Ndugu Jerry Slaa
6. Profesa Anna Tibaijuka
7. Ndugu Stephen Wassira

Wajumbe wa Kamati Kuu - Zanzibar.
1. Ndugu Shamsi Vuai Nahodha
2. Ndugu Hussein Mwinyi
3. Profesa Makame Mbarawa Mnyaa
4. Dokta Salim Ahmed Salim
5. Ndugu Maua Daftari.
6. Ndugu Samia Suluhu Hassan
7. Ndugu Hadija H. Aboud

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad