Meneja Mbunifu wa Ofa za Tigo Tanzania,Suleiman Bushagama (kushoto) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kutambulisha huduma mpya kwa wateja ijulikanayo kama Tigo Time,leo kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.Kulia ni Mbunifu wa ofa za Tigo,Jacqueline Nnunduma na Katikati ni Muwakilishi kutoka Kampuni ya Front Line,Elias Bandeke ambao ni Waratibu wa Mkutano huo.
Mbunifu wa ofa za Tigo,Jacqueline Nnunduma akielezea ofa hiyo mpya kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kutambulisha huduma mpya kwa wateja ijulikanayo kama Tigo Time,leo kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya waandishi wa habari waliofika kwenye mkutano huo.
Tigo imetambulisha huduma mpya kwa wateja ijulikanayo kama Tigo Time, ambayo inatoa punguzo kubwa sana la gharama ya kupiga simu masaa ishirini na nne kwa wiki (24/7 ikitegemeana na muda na wakati wa siku na eneo mteja atakalokuwa.
Kusajili huduma kwa mteja piga *149*90# au tuma neno “TIGO TIME” kwenda namba “15372” na baada ya hapo utapokea ujumbe ambao utaonyesha kwamba umefanikiwa kusajili na unaweza kuanza kutumia huduma hii na ufurahie punguzo kubwa sana la gharama. Baada ya kusajili, Tigo Time itakujulisha punguzo lako la gharama la kupiga simu kutokana na muda wa siku na eneo ulipo. Gharama ya huduma hii ya kusajili itakuwa ni Tshs 149 kwa kiwango cha chini.
“Tigo inatambua kwamba wateja wetu wanahitaji huduma bora na kwa gharama nafuu na hii ni njia mojawapo ya kuhakikisha kuwa wateja wetu wanapata huduma zenye ubora wa juu na vifurushi ambavyo vitawapatia unafuu wa bei kwa muda wowote.” Alisema Bi. Jacqueline Nnunduma, Mbunifu wa ofa za Tigo.
“Kwa punguzo hili kubwa la bei lililopita kifani, hakuna shaka kuwa Tigo Time itakuwa huduma maarufu kama ilivyokuwa huduma ya ya Kwa Sekunde tuliyoianzisha miaka kadhaa iliyopita.” Alimalizia Bi. Nnunduma.
Tigo ni mtandao wa kwanza wa simu za mkononi nchini Tanzania. Ilianza shughuli mwaka 1994 na inapatikana katika mikoa ishirini na sita (26) Tanzania bara na visiwani.
Lengo la Tigo ni kuwa mtandao unaoongoza kwa kutoa huduma bora na za ubunifu Tanzania kwa wateja wake wote ambazo zinaendana na mahitaji yao kuanzia huduma za sauti za bei nafuu, vifurushi vya intaneti vyenye kasi kubwa na huduma bora za fedha za simu za mkononi kupitia Tigo Pesa.
Tigo ni sehemu ya kampuni kubwa ya Millicom International Cellular S.A (MIC) ambayo ni ya unafuu wa huduma na inapatikana kirahisi kwa zaidi ya wateja milioni 43 katika masoko 13 barani Afrika na Amerika ya Kusini.
No comments:
Post a Comment