Wakati Mamlaka ya Mawasiliano Nchini Tanzania (TCRA) juzi iliamua kuingia rasmi katika Mfumo wa Mawasiliano ya Televisheni na Redio kwa kurushwa katika mfumo wa kisasa wa Dijitali kutoka ule mfumo wa Analojia, Shirika la Usambazaji Umeme TANESCO nao wameamua kuingia katika Mfumo huo wa Dijitali kwa staili ya kupandanisha nguzo ya Umeme katika mti halisi ambao bado unamea kama jinsi taswira hizi zinavyoonesha. Taswira hii imepatikana Huko Mkoani Ruvuma, na TANESCO mkoani humo wameamua kutumia njia hii kurahisisha usambazaji umeme.
Jionee jinsi Tanesco walivyo na teknolojia ya kisasa katika kipindi hiki cha Mwaka 2013
Kamba za manila ndizo zilizotumika kuendeleza teknolojia hii ya kisasa kabi na ya Kidigitali.
Kwani kuna utata hapa??
Jiulize kwa hali kama hii Tanesco wako juu kwa mfumo huu au wanajaribu nao mfumo wao mpya?.Picha na Demashonews Blog
No comments:
Post a Comment