HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, January 1, 2013

Sherehe ya Mwaka Mpya kwenye Kumbi za Mango Garden na Green Acress jijini Dar usiku wa Kumkia Mwaka Huu

  Wanenguaji wa Bendi ya Mashujaa, wakishambulia jukwaa, wakati wa onyesho lao lililofanyika wakati wa Mkesha wa mwaka mpya, kwenye Ukumbi wa Green Acres, Victoria jijini Dar es Salaam, mwaka jana kuamkia mwaka huu, kama walivyonaswa na kamera ya sufianimafoto.
 Rapa na mwimbaji waq bendi ya African Stars 'Twanga Pepeta', Kalala Junior, akirap na kumpagawisha mkaanga chips wa bendi hiyo, Martine Kibosho, wakati wa onyesho lao maalum la mkesha wa mwaka mpya, lililokuwa likirushwa Live katika Televisheni ya TBC, jana katika Ukumbi wa Mango Garden Kinondoni, kama walivyonaswa na kamera ya sufianimafoto.
 Mpiga Kinanda wa Twanga, Voctor Mkambi, akiburuza kinanda wakati wa onyesho hilo.
 Rapa na mwimbaji wa bendi ya Mashujaa, Fergason, akighani rap zake huku akitunzwa na mkurugenzi wa bendi hiyo, Mama Sakina, wakati wa onyesho lao la mkesha wa mwaka mpya kwenye Ukumbi wa Green Acres, Victori jana usiku kuamkia mwaka huu.
 Mashabiki wa bendi ya Twanga, wakisebeneka, katika onyesho la bendi yao kwenye Ukumbi wa Mango Garden Kinondoni.
 Kalala  Junior, akiwachezesha mashabiki wake kwa kusugua kisigino jukwaani.
 Kalala Junior, akiwachezesha wanenguaji wake, na sebene la Twanga......
 Wanamuziki wa bendi ya Twanga, wakipozi kwa picha ya kumbukumbu baada ya kushangilia kuukaribisha mwaka mpya na kufungua shampeni.
 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni,Afande Charles Kenyela akizungumza na kutoa salam zake za mwaka mpya za kipolisi baada ya kufunguliwa kwa shampeni na kuukaribisha mwaka mpya, katika ukumbi wa Mango Garden Kinondoni sambamba na bendi ya Twanga iliyokuwa ikirushwa live na TBC.
 Sebene linaendelea......
 Luiza Mbutu (kushoto) na mtangazaji wa TBC (katikati) na shabiki wa Twanga, kwa pamoja wakifungua shampeni kuashiria kuukaribisha mwaka mpya wa 2013, na kuuaga mwaka 2012 wakati wa onyesho maalum la bendi hiyo katika ukumbi wa Mango Garden kinondon usiku wa kuamkia mwaka huu.
 Mashabiki nao wakipongezana kwa kuuona mwaka mpya baada ya kutimu saa sita kamili usiku na kufunguliwa shampeni katika ukumbi wa Mango Garden.
 Luiza Mbutu na Kalala Junior, wakipozi kwa picha mbele ya kamera ya sufianimafoto, baada ya kfungua shampeni kuukaribisha mwaka mpya.
 Shabiki huyu naye hakuwa nyuma kujipa raha mwenyewe, kwa kushangilia na kutingisha bia yake bila kumwaga hata kidogo kama shampeni, ''amwage? hasara ya nani''
 Afande Kenyela, akijumuika na wananchi na wadau wa muziki katika ukumbi wa Mango Garden kinondoni.
 Wanamuziki wa Mashujaa Band, wakishambulia jukwaa wakati wa onyesho lao katika Ukumbi wa Green Acres, Victoria.
 Sehemu ya mashabiki wa bendi ya Mashujaa, wakipata burudani kutoka kwa bendi yao jana usiku wa kuamkia mwaka huu wa 2013.
 Fergason, akiwapagawisha wapiga gitaa wake kwa rap za bendi hiyo......
Mama Sakina, akifurahia na kucheza sebene la bendi yake wakati wa onyesho lao katika ukumbi wa Green Acres, Victoria usiku wa kuamkia mwaka huu wa 2013. Picha Zote na www.sufianimafoto.blogspot.com

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad