Waombolezaji wakiwa wamejipaga tayari kwa kuupokea Mwili wa Marehemu Sadick Juma Kilowoko (SAJUKI) mchana wa leo kwenye Makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam.
Rais Jakaya Kikwete (wa pili kulia) akiwa katika Mazungumzo na Baba Mzazi wa Marehemu Sadick Juma Kilowoko,Mzee Juma Kilowoko,Meya wa Manispaa ya Ilala,Mh. Jerry Silaa (kulia) na Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania,Saimon Mwakifwamba Mara baada ya Mazishi wa Msanii wa Filamu,Marehemu Sadick Juma Kilowoko (SAJUKI) yaliyofanyika mchana wa leo kwenye Makaburi ya Kisutu,jijini Dar es Salaam.
Rais Jakaya Kikwete akiwa katika Mazungumzo na Meya wa Manispaa ya Ilala,Mh. Jerry Silaa (kulia) na Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania,Saimon Mwakifwamba wakati wa Mazishi wa Msanii wa Filamu,Marehemu Sadick Juma Kilowoko (SAJUKI) yaliyofanyika mchana wa leo kwenye Makaburi ya Kisutu,jijini Dar es Salaam.
Rais Jakaya Kikwete akimsiliza kwa makini Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania,Saimon Mwakifwamba.
Waombolezaji wakiwa Makaburini.
Mh. Zitto Kabwe akiwa katika Mazungumzo na Wadau.
Mh. Iddi Azzan akizungumza na Mwandishi wa habari wa Gazeti la Tanzania Daima,Andrew Chale.
Mpiga Picha wa Gazeti la Uhuru,Akimapa taswira yake Maridhawa wakati wa Mazishi wa Msanii wa Fimalu,Marehemu Sadick Juma Kilowoko (SAJUKI) Makaburi ya Kisutu jijini Dar leo.(halafu unaona mtu hapa anavyotafuta picha zake kwa mbinde,baadae unakuwa watu wengine bila haya wanakopi na kuweka kwenye vyombo vyao vya habari tena bila hata kusema wametoa wapi,wakijidai wamepiga wao.yaani sio fea kabisaaaaa na tunarudishana nyuma)
Wadau mbali mbali wakiwa makaburini.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh. Jakaya Mrisho Kikwete akiweka udongo kwenye Kaburi la Marehemu Sadick Juma Kilowoko (SAJUKI) wakati wa Mazishi yake yaliyofanyika mchana huu kwenye Makaburi ya Kisutu,Jijini Dar es Salaam.
Mwili wa Marehumu Sadick Juma Kilowoko ukiwasili kwenye Makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam leo tayari kwa Mazishi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh. Jakaya Mrisho Kikwete akiweka udongo kwenye Kaburi la Marehemu Sadick Juma Kilowoko (SAJUKI) wakati wa Mazishi yake yaliyofanyika mchana huu kwenye Makaburi ya Kisutu,Jijini Dar es Salaam.
nampongeza Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania kwa kujitoa kwake katika jamii bila kujali wewe ni maskini au tajili kwa kweli kama binadamu anamapungufu yake mengi tu lakini kwa moyo anaouonyesha kwa kujishusha bila kujikweza na kujiona wa maana na kuamua kutoa ushirikiano katika kila matatizo yanapotokea nampongeza sana na kumuombea kwa Mungu AZIDI KUMBARIKI NA KUMPA HEKIMA YA KUIONGOZA TANZANIA
ReplyDeleteMUNGU IBARIKI TANZANIA MUNGU MBARIKI RAIS WETU JAKAYA MRISHO KIKWETE
inatia uchungu kweli unaweza usiamini kama sajuki ndio safari yake ya Mwisho amepumzishwa leo kwenye nyumba yake ya milele.Mungu akupe nguvu mwanamke ambaye ni mfano wa kuigwa Wastara ila wasanii mjifunze mpendane muungane kweli msaidiane kwenye shida na raha.Kweli nimeamini Sajuki alikuwa mtu wa watu wainnallilah wainnallilah rajuni
ReplyDeletemama liz.arusha
mdau wa kwanza na mimi naungana na wewe kumpongeza rais kwa kweli anajitahidi sana kujitoa hata kwa watu wa kawaida sana! Mungu ambariki kwa kweli...
ReplyDeleteNAUNGANA NA MDAU WA KWANZA NA MIMI NAMPONGEZA KWA MOYO WAKE WA UPENDO NA HURUMA ANAONYESHA KWA WATU WAKE,MUNGU AKUBARIKI SANA RAIS WETU ,MUNGU IBARIKI TANZANIA NA WATU WAKE.
ReplyDeleteMAMA lINDA TBT
mungu amlaze mahali pema peponi amin na kumpongeza kikwete kwa ushirikiano wake hongera sana kikwete aendelee kujichaganya na watu watanzania wake
ReplyDeletelily e mic
Jerry Silaa huwezi kusimam hadi ukae kwenye kiti wakati wewe kijana?pia umejaza mabango kila kona ya Dar anapopita Rais ukijitangaza huku ukitumia jina la rais wetu eti unampa hongera.ya kuwa mwenyekiti.hilo sio tatizo lakini kwenye hayo mabango unaweka jina lako.tena kwa herufi kubwa.wakati ulitakiwa uweke nembo ya Manispaa.
ReplyDelete